Wanasayansi
na mambo yao! mh.
Kitengo
cha utafiti wa kilimo nchini Kenya kijulikanacho kama Kenya Agricultural
Research Institute (KARI)chini ya mtafiti Phoebe Mukiria aliwaeleza jopo la waandishi
habari mjini Nairobi yakwamba wamekuja na utafiti ambao utakua ni mkombozi kwa
watu wenye vidonda ndugu na vinavyochukua muda mrefu kupona
Hata
hivyo Phoebe ameweka kituo kwamba watatoa ithibati yao juu ya matumizi funza
ama mabuu katika kuponyesha madonda sugu wenye uwezo wa kusafisha na kuponya
kabisa ndani ya miezi mitatu.
Warsha
hiyoiliyochukua muda wa siku tatu iliwakutanisha washiriki wapatao 200 ambao
walikua na jukumu la kujadili namna ambavyo funza ama mabuu hayo yatakavyowekwa
katika ngozi ama nyama za mwili zenye
kidonda hicho, na baada ya wadudu hao kufanya kazi yao basi ndipo madaktari wa
upasuaji watakapo endelea na taratibu zao za matibabu kwa mgonjwa.
Bi
Phoebe ameongeza kwamba, mabuu ama funza hao huwa chukua siku kumi kuweza
kusafisha eneo husika,ama athari kama ni kubwa basi wadudu hao wanaweza kutumia
hadi mwezi kutibu/
Inasemekana,
Utafiti huo umeleta mafanikio makubwa baada ya kufanya majaribio kwa watu 5
ambao wameonesha mafanikio baada ya funza hao kuondoa ngozi iliyooza katika
vidonda vyao.
Majaribio
hayo yamefanywa kati ya vyuo vikuu vya Nairobi, KARI, chuo kikuu cha Slovakia Comenius University pamoja na Tenwek Mission Hospital in Kenya.
Watafiti
hao wameomba ridhaa ya serikali wafanye utafiti zaidi kwa mwaka mmoja ujao,na
watawafanyia utafiti watu wenye vidonda sugu ya vidonda, wagonjwa wa kisuka na
kueleza wazi utunzani na matibabu ya vidonda ni ghali.
Kwa
muujibu wa Mukiria, utabibu huo hautafanywa
kwenye vidonda vilivyoko kwenye mirija mikubwa ya damu na wadudu hao
wameonyesha mafanikio makubwa ya matibabu katika sehemu zingine za mwili, na
kuowaondoa hofu watu kua matibabu haya katika nchi zilizoendelea ni jambo la
kawada kuwatibu wanyama wafugwao, na pindi watakapopewa ridhaa waiombayo basi
huduma zao watazitanua wigo mpaka kwa wanayama.
No comments:
Post a Comment