Rais Uhuru Kenyatta
ameipongeza kampuni ya China kwa kuweza kukarabati bure uwanja wa ndege wa Jomo
Kenyatta ndani ya wiki tatu baada ya uwanja huo kukumbwa na ajali ya moto
mwanzoni mwa mwezi uliopita.
Kampuni hiyo kutoka
China imeweza kujenga kituo kimoja cha muda cha ndege kwa gharama ya dola
milioni 1 za kimarekani bila malipo kutoka kwa serikali ya Kenya.
Baada ya kukagua uwanja
huo, rais Kenyatta ameeleza kuridhika kwake na huduma kurudi katika hali ya
kawaida kwenye uwanja huo, na kutaja kituo hicho cha muda kama "zawadi kwa
Wakenya".
Ameongeza kuwa huku
uwanja huo ukiendelea kupanuliwa kwa sasa, unatarajiwa kuwa kituo muhimu cha
safari kwa bara zima la Afrika.
Uwanja huo wa ndege
ambao ni mkubwa zaidi katika Afrika mashariki na kati ulikumbwa na ajali ya
moto tarehe 7 mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment