Monday, September 23, 2013

SHAMBULIZI LA KIGAIDI LA AL SHABAAB HUKO KENYA





Mtoto akimkimbilia askari ili kuokolewa



Septemba 21, mwaka huu ni tarehe ambayo Kenya haitaisahau kamwe. Ni baada ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabab lilipoishambulia mall ya Westgate maarufu kwa kuwa na wateja matajiri jijini Nairobi ,Al-shabab iliamua  kuwashikilia watu mateka, kuwaua na kuwajeruhi wengine

Mwanaume huyu inaaminika alipigwa risasi na kufa akiwa ameketi kwenye gari.

Mama huyu akiwa katika taharuki baada ya kujeruhiwa, na alikua katika hali ya kuhitaji msaada wa haraka.
Familia ikiwa imeshikana mikono kuitoka Westgate Mall.
Mwinda, huwindwa, askari akiwalia timing magaidi wa kundi la  A-Shabb.
Dada huyu akisaidiwa baada ya kunusurika.
Mama na wanawe wakiwa wamelala chini ili kujinusuru.

Dada huyu haamini kua yuko nje ya WestgateMall, yu hoi kwa taharuki,pumzi zimempaa.

Mfanyakazi wa Red Cross akiwa amembeba mtoto aliyekuwa ndani ya mall hiyo.

Mtoto akiwa amesimama pembeni ya maiti ya mtu,mtoto huyo alikua ndani ya Mall hiyo.

Hakika walipendana mpaka kifo, wapenzi wawili walipigwa risasi na wanamgambo wa A-Shabab na kufa wakiwa wamekumbatiana! Huzuni iliyoje!

Ilibidi chochote kitumike kama nyenzo ya kuwanusuru manusura.

Yuko kwenye mikono salama, lakini analia nab ado amejisalimisha, usiombee yakukute, yasikie tu haya mambo.

Ni vilio tupu!  Westgate Mall ama vya furaha,ama shukurani  kwa Mungu!
 Askari huyu amejeruhiwa tumboni lakini kifaa chake cha kazi bado anacho ilhali amekamatia tumbo  kwa mkono mmoja.
Askari  wakiingia katika jengo hilo
Kama movie vile! kila lakheri ingawa hamna vifaa vya kujikingia.
Dada huyu  Raia wa Canada Annemarie Desloges, alokua na miaka 29 alipigwa risasi na kufa.
Wananchi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shopping kwenye mall hiyo wakiambiwa kuinua mikono yao kuonesha hawana silaha ,Gaidi mmoja alikamatwa jana na kufa kutokana na majeraha. Maafisa wa Kenya wameiambia BBC kuwa wengine wanne wamekamatwa



No comments:

Post a Comment