ligi za soka barani ulaya ziliendelea mwishoni mwa wiki hii kwa
michezo iliyopigwa kwenye viwanja tofauti .katika mchezo wa kwanza uliopigwa
huko england mabingwa watetezi wa ligi hiyo manchester united waliwafunga
vijana waliopanda daraja crystal palace mabao mawili bila .mabao ya united kwenye
mchezo huo yalifungwa na washambuliaji robin van persie na wayne rooney.
KWINGINEKO ARSENAL WALIWAFUNGA SUNDERLAND 3-1 KATIKA MCHEZO ULIOPIGWA KWENYE UWANJA WA
NYUMBANI WA SUNDERLAND THE STADIUM OF LIGHT .
ARSENAL WALIFUNGA KUPITIA KWA OLIVIER GIROUD NA AARON RAMSAY
ALIYEFUNGA MABAO MAWILI HUKU CRAIG GADNER AKIFUNGA BAO LA SUNDERLAND
Newcastle united waliwafunga aston villa 2-1 huku wafungaji
wakiwa hatem ben arfa na yoan goufran kwa newcastle na christian benteke akifunga
bao pekee la villa . Tottenham hotspurs waliwafunga norwich city 2-0 . mabao ya
spurs yalifungwa na gylfi siggurdson ambaye alifunga mabao yote mawili .
MECHI
YA HULL CITY NA CARDIFF CITY TIMU MBILI AMBAZO ZIMEPANDA DARAJA MSIMU HUU ILIISHA
KWA SARE YA 1-1 . HULL WALIANZA KUFUNGA KUPITIA KWA CURTIS DAVIES KABLA YA
PETER WITTINGHAM HAJAISAWAZISHIA CARDIFF CITY KWENYE KIPINDI CHA PILI .
FULHAM
NA WEST BROMWICH ALBION NAO WALITOKA SARE YA 1-1 . WAFUNGAJI KWENYE MCHEZO HUO
WALIKUWA STEVE SIDWELL KWA FULHAM NA GARETH MCAULEY KWA WEST BROM.KATIKA MCHEZO WA MWISHO
KWA SIKU YA JUMAMOSI CHELSEA WALIKUBALI KIPIGO CHA BAO MOJA BILA TOKA KWA
EVERTON . BAO PEKEE LA MCHEZO HUO LILIFUNGWA NA STEVEN NAISMITH .
NCHINI HISPANIA MABINGWA WATETEZI WA LIGI FC BARCELONA
WALIWAFUNGA FC SEVILLA KWA TATU KWA MABAO MATATU KWA MAWILI . MABAO YA BARCA
YALIFUNGWA NA DANI ALVES , LIONEL MESSI NA ALEXIS SANCHEZ HUKU IVAN RAKITIC NA
ANDUJAR WAKIWAFUNGA MABAO YA SEVILLA.
VILLAREAL AMBAO WAMEPANDA DARAJA MSIMU HUU WALIWABANA REAL
MADRID NA KUWALAZIMISHA SARE YA MABAO MAWILI KWA MAWILI . REAL MADRID WALIFUNGA
MABAO YAO KUPITIA KWA MCHEZAJI WAO MPYA GARETH BALE NA CRISTIANO RONALDO
AKIFUNGA BAO LINGINE HUKU CANI PAMOJA NA GIOVANI DOS SANTOS WAKIFUNGA MABAO YA
VILLAREAL.
NAO ATLETICO MADRID WALIWAFUNGA ALMERIA MABAO MANNE KWA
MAWILI.WAFUNGAJI WA ATLETICO KWENYE MCHEZO HUO WALIKUWA DAVID VILLA , DIEGO
COSTA , KOKE NA TIAGO MENDEZ .NCHINI ITALIA MABINGWA WATETEZI JUVENTUS NA INTER
MILAN WALITOKA SARE YA BAO MOJA KWA MOJA .
INTER WALIANZA KUFUNGA KUPITIA KWA MAURO ICARDI NA JUVENTUS
WALISAWAZISHA KUPITIA KWA ARTURO VIDAL.FIORENTINA NA CAGLIARI NAO WALITOKA SARE
YA BAO MOJA KWA MOJA . MABAO KWENYE MCHEZO HUO YALIFUNGWA NA BORJA VALERO KWA
FIORENTINA NA MAURICIO PINILLA KWA CAGLIARI.
KWENYE LIGI YA UJERUMANI BORRUSIA DORTMUND WALIWAFUNGA HAMBURG
SV MABAO SITA KWA MAWILI . WAFUNGAJI WA DORTMUND WALIWAKUWA PIERRE EMERICK
AUBAMEYANG NA ROBERT LEWANDOWSKI AMBAO WALIFUNGA MABAO MAWILI KILA MMOJA MARKO
ROIS NA HENRI KITARAYAN HUKU HAMBURG WAKIFUNGA KUPITIA KWA ZHI GI LAM NA HEIKO
VESTERMAN.
BAYERN MUNICH WALIWAFUNGA HANNOVER 96 MABAO MAWILI BILA .
WAFUNGAJI KWENYE MCHEZO HUO WALIKUWA FRANK RIBERY NA MARIO MANZUKICH.NCHINI
UFARANSA PARIS ST GERMAIN WALIWAFUNGA BORDEAUX MABAO MAWILI BILA . MABAO YA
MCHEZO HUO YALIFUNGWA NA BLAISE MATUIDI NA LUCAS MOURA.
MONACO AMBAO WANAONGOZA LIGI YA UFARANSA WALISHINDA MCHEZO WAO
DHIDI YA LORIENT KWA BAO MOJA BILA . BAO PEKEE LA MCHEZO HUO LILIFUNGWA NA
RADAMEL FALCAO.
No comments:
Post a Comment