Japan
imeonja ushindi wa kinyang'anyiro cha kuandaa Michezo ya Olimpiki mwaka wa
2020, ikitarajia kuimarika uchumi wake baada ya miongo miwili ya kudorora
kutokana na athari za tetemeko la ardhi Tsunami.
Rais wa timu za Michezo ya Olimpiki ya Ujerumani na ambaye ni mgombea wa
wadhifa wa Urais wa Kamati ya Olimpiki Duniani IOC Thomas Bach.
Rais
wa timu za Michezo ya Olimpiki ya Ujerumani na ambaye ni mgombea wa wadhifa wa
Urais wa Kamati ya Olimpiki Duniani IOC Thomas Bach, anaelezea sababu
zilizochangia kuchaguliwa mji wa Tokyo kama mwenyeji wa Mashindano ya Olimpiki
2020.
"Tokyo , kwa mtazamo wa wanachama wa IOC, katika hali hii tete ya
dunia, inaangaliwa kama mahala salama,kwa kuzingatiwa pia desturi fulani za
kutoa maombi. Wameboresha tena maombi yaao tangu walipoyatuma. Wanadhaamini utulivu
upande wa fedha na pia upande wa kisiasa.Nnaamini hoja zote hizo zimechangia
kuiona hatimae Tokyo ikiangaliwa kama mahala tulivu na salama kuliko kote
kwengine."
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe.
Waziri
Mkuu wa Japan Shinzo Abe alijihusisha moja kwa moja katika juhudi za kuufanya
mji wa Tokyo kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya Olimpiki, na sasa anafahamu
kibarua kilichopo cha kujiandaa kikamilifu kwa tamasha hilo. Abe amesema
"Tungependa kuwashukuru wale wote waliouunga mkono mji huu. Wacha
nimsalimu kila mtu aliyefanya juu chini katika kinyang'anyiro hiki, kama vile
Uhispania na Uturuki.
Kimekuwa kinyang'anyiro kirefu na kigumu na ningependa
kuwapongeza wanamichezo wote pamoja na Gavana wa Tokyo na wanariadha, kwa
kusaidia katika juhudi za kuandaa Michezo ya Olimpiki. Bila juhudi zao
hatungelishinda ombi hili. Sasa, kazi halisi inaanza. Tutaanza maandalizi, kwa
Michezo ya Olimpiki na Olimpiki ya walemavu jijini Tokyo 2020 ili iwe yenye
mafanikio".
kama
wewe ni mpenzi wa mchezo wa mieleka, au kama wewe ni mwanamieleka, basi una
sababu ya kuanza kujiandaa, kwa sababu mchezo huo umeongezwa katika orodha ya
michezo itakayoshirikishwa katika mashindano ya Olimpiki mwkaa wa 2020 na 2024.
Mchezo wa Mieleka ulipigiwa kura na kuishinda michezo ya baseball na squash
baada ya mchezo huo wa jadi kufanyiwa mageuzi makubwa tangu ulipoondolewa kwa
muda mwezi Februari. Mchezo wa mieleka ulipata kura 49 miongoni mwa wanachama
95 wa Kamati ya Kimataifa ya Ompiki – IOC.
Nenad Lalovic
Rais
wa Kamati ya Maamuzi katika spoti FILA, Nenad Lalovic amesema mieleka siyo
mchezo mpya, lakini mara hii wanaleta aina mpya ya mieleka. Kwamba wamejaribu
kuuimarisha mchezo huo na kuufanya kuwa wa kuburudisha na kuwasisimua zaidi
mashabiki. Kamati ya Michezo ya Olimpiki iliongeza Rugby na Gofu kwenye
mashindano ya mwak wa 2016 mjini Rio. Michezo hiyo pamoja na Mieleka sasa
inafikisha 28 jumla ya michezo katika mashindano ya Olimpiki.
No comments:
Post a Comment