Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 4 ,raia wa Uingereza ambaye alinaswa katika jingo la westgate Mall alionesha ushupavu wa ajabu pale alipomkabili mwanamgambo wa alshabab alokua na bunduki na kumpa ya moyoni mwake kwa kumwambia kua ye si mtu mzuri ,mwanamgambo huyo yalimuingia moyoni maneno hayo na kumuomba msamaha motto huyo, imefahamika leo
Elliot Prior, kutoka Windsor,huko Berkshire,alifunguka kwa kumtetea mamake mzazi aitwaye ,Amber,ambaye alipigwa risasi mguuni wakati dada wa mtoto huyo Amelie akishuhudia kila kitu .
Cha ajabu wana mgambo hao hawakujali wala nini baadae waliwaachilia watoto hao namama yao lakini wakawapa watoto hao biskuti aina ya Mars na kuwaambia: 'Please forgive me, we are not monsters.'
Amber ni film producer,na aliingia Westgate Mall akakuta foleni katika duka aliloliendea kununua maziwa ya wanawe wawili,akajiunga katika foleni na muda si muda yakaanza majanga ya kurushiwa risasi.
Mapigano baina ya wanamgambo hao wa Al-Shabab na askari pamoja na wanajeshi wa serikali ya Kenya yameingia katika siku ya nne leo, na ndipo tunapata habari hii ya kusisimua.
Pamojana kwamba askari polisi wa Kenya kutoa maelezo kwamba wameidhibiti Westgate Mall ,na mawasiliano baina ya walio nje na ndani ya jingo hilo yanasema kwamba bado mateka 10 hadi 13 wana shikiliwa na magaidi hao.
Kitu kingine cha kusikitisha picha ya Amelie ilinishangaza mwanzoni nilipoiona nisijue ameshika nini kumbe Mars bars alizopewa na mwanamgambo wa Al-Shabab akiwa amesimama pembeni ya maiti ya mwanamume baada ya kua wamenusuriwa na wauaji hao
No comments:
Post a Comment