Italia, Ujerumani na
Uholanzi na Uhispania zinaweza kujipa nafasi ya kushiriki katika Dimba la Dunia
mwaka wa 2014 wakati timu za Ulaya zitakapoingia viwanjani tena Jumanne
10.09.2013 kwa mechi za kufuzu.
Miamba wote wa soka
barani Ulaya wamejiimarisha kileleni mwa makundi yao na watalenga kuepuka
masaibu katika dakika za mwisho mwisho kwa kujikatia tikiti zao wakati kukiwa
kumesalia mechi kadhaa za kuchezwa.
Italia itapata nafasi
ya kwanza katika kundi B kama itashinda nyumbani mchuano wao na Jamhuri ya
Czech lakini Wajerumani na Waholanzi wanahitaji ushindi dhidi ya Visiwa vya
FAROE na Andorra, na pia wakitaraji kuwa matokeo ya mechi nyinegine yatawaendea
ili
wafuzu moja kwa moja.
Ujerumani itatalenga kuwafunga WaFaroe mabao mengi
lakini itajihakikishia nafasi tu ya kuongoza kundi C na kujipa tikiti ya 16
mfululizo ya kushiriki dimba la dunia kama nambari mbili Sweden watashindwa na
Kazakhstan.
Mshambuliaji chipukizi
wa Ujerumani Marco Reus atakosa mchuano dhidi ya Visiwa vya Faroe Mshambuliaji
chipukizi wa Ujerumani Marco Reus atakosa mchuano dhidi ya Visiwa vya Faroe.
Uholanzi pia ni lazima
iwaangamize Andorra ambayo haina pointi hata moja wala bao, kufikia sasa katika
kundi D lakini inataraji kuwa nambari mbili Romania itadondosha pointi nyumbani
itakapocheza na Uturuki. Mambo ni magumu zaidi hata kwa timu ya England, ambayo
inaongoza kundi H lakini huenda ikatafuta tikiti yake kupitia mechi za mchujo
kama itashindwa kutoka mjini Kiev, Ukraine na angalau pointi moja katika mechi
hiyo kali ya kufuzu.
Ukraine iko katika
nafasi ya tatu na tofauti ya pointi moja na italenga kuipindua England kama
itaweza kulipiza kisasi kichapo dhidi ya wapinzani hao katika mchuano wa
makundi wa dimba la mataifa ya bara Ulaya UEFA Euro mwaka jana mjini Donetsk.
Katika mechi nyingine,
Ufaransa ambayo matumaini yake yanadidimia, itachuana na Belarus, wakati Urusi
ikiibandua uongozini Ureno katika kundi F kama itaishinda Israel ikiwa na
mchuano mmoja wa ziada. Uswisi huenda ikapunguza uongozi wake wa kundi E kwa
pointi moja kama itashindwa na Norway mjini Oslo. Bosnia-Herzegovina na Ugiriki
zinaongoza kundi G na pointi 16 kila mmoja na zitamenyana na Slovakia na
Latvia.
Tukiangalia Amerika ya
Kusini, Argentina na Colombia zinaweza kujikatia tikiti hapo kesho. Timu hizo
mbili zinaongoza kundi la nchi za Amerika ya Kusini zikiwa na pointi 26
kutokana na mechi 13. Argentina ambayo ina faida ya pengo kubwa la mabao,
inaweza bado kufuzu hata kama itashindwa ugenini Paraguay, wakati sare yoyote
nchini Uruguay ikitosha kuwapa Colombia nafasi ya kucheza katika Kombe la Dunia
kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1998.
Timu nne zitafuzu moja kwa moja kutoka
Amerika ya Kusini, pamoja na nafasi ya kupata timu ya tano kupitia mechi ya
mchujo dhidi ya timu ya bara Asia. Wenyeji Brazil walipewa tikiti ya moja kwa
moja. Chile ni ya tatu na pointi 24 baada ya mechi 14, wakati Equador ikiwa
ikiwa ya nne na pointi 21. Uruguay ni ya tano na pointi 19. Venezuela na Peru
zina nafasi ndogo za kusafiri nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment