Mkurugenzi wa Uvinza Fm Ayubu Kalufya
akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Khadija Nyembo kwa Meneja
wa Mradi wa Demokrasia na Amani kutoka UNESCO Courtney Ivins mara
baada ya kuwasili kwenye halfa ya kuzindua Mradi Wa UNESCO – UNDP wa
kuhamasisha Amani katika mchakato wa kukuza Demokrasia katika kipindi
hiki cha kuelekea uchaguzi mwaka 2015 uliofanyika kwenye Kituo
tarajiwa cha Redio ya Jamii Uvinza Fm Wilayani
Uvinza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uvinza Fm Nuru Kalufya (wa pili
kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Khadija Nyembo
mara baada ya kuwasili.
Mkurugenzi wa Uvinza Fm Ayubu Kalufya
akitambulisha meza kuu kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuzindua
mradi wa UNESCO-UNDP wa kuhamasisha Amani katika mchakato wa kukuza
Demokrasia katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mwaka
2015.
Meneja wa Airtel mkoani Kigoma Philip Nkupama
akiwasalimia wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye hafla ya uzinduzi
wa mradi huo uliofanyika kwenye kituo cha
vijana Uvinza mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uvinza Fm Nuru Kalufya
akiwasalimia wageni waalikwa kwenye uzinduzi
huo.
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Khadija Nyembo akiteta
jambo na Mtaalamu mhandisi wa mitambo na mafunzo ya awali kwa
watangazaji wa redio Uvinza Fm kutoka nchini Aurstralia Bw. Rukmin
Wijemanne
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Mwl.
Khadija Nyembo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni
Kanali Mstaafu Issa Machibya wakati akizundua mradi wa UNESCO-UNDP wa
kuhamasisha Amani katika mchakato wa kukuza Demokrasia
katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mwaka 2015
uliofanyika kwenye Kituo tarajiwa cha Redio ya Jamii
Uvinza Fm Wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
Sehemu ya wageni waalikwa na waandishi wa habari
watarajiwa wa Redio Uvinza Fm wakimsikiliza mgeni
rasmi.
Meneja wa Airtel mkoani Kigoma Philip Nkupama
akizungumza nia yao ya kutoa ufadhili kwa Redio Uvinza Fm kurusha
matangazo yao kupitia minara ya Airtel ambapo pia amesema lengo lao ni
kusaidia jamii zilizo na changamoto mbalimbali ikiwemo za mila potofu,
Elimu duni, Ukeketwaji, imani za kishirikina, maendeleo duni ,
ukandamizaji wa Wanawake na Watoto na changamoto nyingine
nyingi.
Ameongeza kuwa kupitia mradi wa Redio Jamii,
Jamii itafikishiwa taarifa zote pamoja na kupambana na changamoto
mbalimbali nchini kwenye Siasa, Uchumi na Utamaduni na wakati huo huo
kuiongezea jamii ufahamu kuhusu hali ya mwelekeo wa nchi yao kwa
ujumla.
Kikundi cha kinamama cha Uhamasishaji cha
Warumba wilayani Uvinza kikitoa burudani wakati wa hafla
hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwl. Khadija Nyembo (wa
tatu kushoto) akishiriki kucheza ngoma za asili na kinamama wa
kikundi cha uhamasishaji wilayani humo Warumba wakati wa hafla
hiyo.
Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama
Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo mbele ya mgeni rasmi jinsi
atakavyoendesha mafunzo hayo kwa waandishi na watangazaji watarajiwa
wa Redio Uvinza Fm ambapo masomo hayo yatagusa nyanja mbalimbali
ikiwemo habari ni nini, mbinu za kuibua habari, habari na
jinsia na kuelimisha jamii. Watajifunza pia jinsi ya kuhariri habari,
miundo mbalimbali ya vipindi kwa mujibu wa mwongozo mamlaka ya
mawasiliano Tanzania-TCRA,’
Meneja wa Mradi wa Demokrasia na Amani kutoka
Unesco Courtney Ivins akifafanua jinsi mradi huo utakavyotekelezwa na
Redio za Jamii nchini kuelekea uchaguzi mwaka
2015.
Kundi la Black and White kutoka wilayani Uvinza
likitoa burudani ikiwa ni fundisho kwa mambo yanayojitokeza wilayani
humo lakini hayana mahali pa kusemewa, Redio Uvinza itasaidia
kukomesha matukio kama hayo ya ukabaji.
Baadhi ya madiwani wa Wilaya ya Uvinza
waliohudhuria uiznduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa Redio Uvinza Fm
wakisaidiana kubeba mitambo mipya ya Redio ya Jamii Uvinza Fm
iliyotolewa na shirika la UNESCO kwa kushirikiana na
UNDP.
Mtaalamu mhandisi wa mitambo na mafunzo ya awali kwa
watangazaji wa redio Uvinza Fm Bw. Rukmin Wijemanne akihakiki mitambo
ya Redio hiyo kama imekamilika tayari kuifunga. Kulia ni Meneja wa
mradi wa DEP Courtney Ivins akikagua maboksi ya vifaa
hivyo.
Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama
Rose Haji Mwalimu, Meneja wa Airtel mkoani Kigoma Philip Nkupama
wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi na watangazaji watarajiwa
wa Redio Uvinza Fm.
Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama
Rose Haji Mwalimu akiagana na Meneja wa Airtel Mkoani Kigoma Philip
Nkupama aliyeambatana na Mratibu wa Maendeleo ya Biashara wa Airtel
mkoani Kigoma Bw. Samwel Lumanyisa mara baada ya kuhitimisha hafla ya
uzinduzi wa mradi huo.
Na Mwandishi Wetu
Serikali inakaribisha miradi ya kuhamasisha
amani katika mchakato wa kukuza demokrasia katika kipindi hiki cha
kuelekea uchaguzi mwaka 2015 inayozingatia habari za uhakika na
maadili ya kiafrika kupitia radio za kijamii.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Bi Khadija Nyembo kwenye hafla ya
uzinduzi wa mradi wa shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na
utamaduni (UNESCO) wakishirikiana na shirika lingine la umoja wa
mataifa la programu za maendeleo (UNDP) amesema mradi huu wa amani
unahamasisha jamii umuhimu wa amani ili kukuza demokrasia
nchini.
“mafunzo ya mafundi mitambo yanayoendeshwa na
mtaalamu mhandisi wa mitambo kutoka Australia pamoja na mafunzo ya
awali kwa watangazaji wa redio kituoni hapa na wale maripota wa
kujitolea kutoka baadhi ya vijiji na kata ambazo redio hii ya Uvinza
FM itasikika, ni mafanikio makubwa kwa maendeleo ya wilaya ya Uvinza
na mkoa wa Kigoma kwa ujumla,” amesema Kiongozi
huyo.
Amesema wanahabari watakaoshiriki katika warsha
hii ya siku tano watajifunza na kufanya mazoezi katika mada za
kitaaluma pamoja na kanuni za maadili katika kutafuta na kuripoti
habari.
“watajifunza habari ni nini, mbinu za kuibua
habari, habari na jinsia na kuelimisha jamii. Watajifunza pia jinsi ya
kuhariri habari, miundo mbalimbali ya vipindi kwa mujibu wa mwongozo
mamlaka ya mawasiliano Tanzania-TCRA,’
amefafanua.
Bi Nyembo amesema Kampuni ya simu za viganjani
ya Airtel imetoa msaada kwa kuruhusu minara yake itumike kurushia
matangazo kutoka kituo cha Uvinza FM Radio kwa upande mmoja na kwa
upande mwingine wanashirikiana na serikali za mitaa katika kufanikisha
mradi huo.
Amesema kitendo cha halmashauri ya wilaya ya
Uvinza na halmashauri ya kijiji cha Uvinza kwa pamoja kutoa sehemu
moja ya jengo la vijana kwa ajili ya Uvinza FM Radio ni jambo la
kuigwa katika jamii kwa ujumla.
“Kwa niaba ya serikali yote hapa mkoani kwa
ujumla natoa pongezi zangu za dhati kwa wadau hao wote waliowezesha na
watakaowezesha ukamilishaji wa mtambo huu na pia kuendeshwa kwa mradi
huu wa UNESCO-UNDP wa uhamasishaji wa amani katika mchakato wa
demokrasia kuelekea uchaguzi 2015.
“Kwa mujibu wa UNESCO mradi huu utazihusisha
redio 26 zilizoko Tanzania bara na visiwani. Kati ya redio hizo tatu
mpya zitajengwa na kuanzishwa Micheweni Pemba, Tumbatu Unguja ikiwemo
Uvinza FM redio jamii Tanzania bara. Ni jambo la
kujivunia,”.
No comments:
Post a Comment