Wednesday, September 11, 2013

MTI WASHANGAZA WAKAZI KWA ‘KUKATAA KUKATWA’ MURANG'AMwanamke akusanya kuni kutoka kwa mti wa mtini (Mugumo) ambao ulianguka baada ya mvua kubwa kunyesha kijiji cha Giakanja, Nyeri .Mwanamke akusanya kuni kutoka kwa mti wa mtini (Mugumo) ambao ulianguka baada ya mvua kubwa kunyesha kijiji cha Giakanja, Nyeri .

Mwanamke akusanya kuni kutoka kwa mti wa mtini (Mugumo) ambao ulianguka baada ya mvua kubwa kunyesha kijiji cha Giakanja, Nyeri .
WAKAZI wa kijiji kimoja Kaunti ya Murang’a wameshangazwa na mti mmoja wa Mugumo ambao 'umekataa’ kukatwa.
Wakazi hao wa kijiji cha Gitura eneo bunge la Kandara wanadai wamejaribu mara saba kuukata mti huo ambao wanasema umekuwa hapo kwa karibu miaka 300.Walisema mwanamme mmoja aliaga dunia hivi majuzi na mkewe kuwa mwenda wazimu baada ya jamaa huyo kuchanja kuni kutoka kwenye mti huo na kuziuza.
Wakielezea wasiwasi wao, wakazi hao walisema mashoka na mapanga huisha makali punde tu wanapojaribu kuuangusha mti huo.Kulingana na tamaduni za jamii ya Agikuyu, mti wa Mugumo ni mtakatifu na haufai kukatwa kamwe.
Vile vile wazee wa jamii hiyo hufanya maombi maalum na matambiko chini ya mti huo.Kulingana na chifu  wa Lokesheni ya Gitura Bw Joseph Kahura,mwanamume huyo alikata kuni na kufaa na mkewe ikabidi apelkwe hospitali ya magonjwa ya ubongo Mathari Mjini Nairobi.
“Tumejaribu kuukata mti huu mara saba naa haukatiki na tunaona unahatari ya kuwangukia wakazi,” alisema Bw Kahura.Naye Mzee mmoja wa kijiji hicho Bw Kamau Kuria alisema hata mti huo ukiangushwa na upepo au mvua, kuni zake hazifai kutumiwa bila idhini ya wazee.

HATARI“
Hakuna mtu yeyote amekubaliwa kuukata mti wa Mugumo bila idhini na anayefanya hivyo hufa au hupatwa na janga,” alihoji.
Mbunge wa eneo hilo Bi Alice Wahome aliomba serikali kusaidia jamii hiyo kuukata mti huo akisema mti huo ni hatari kwa wakazi na mwenye shamba hilo ambapo mti umemea angetaka kulilima.Huenda serikali ndiyo itakayomudu kuuangusha mti huo ikiwa itamudu kufanya hivyo, jambo wanalodai wakazi kuwa ni muhimu kwao.

1 comment: