Wednesday, September 11, 2013

KESI YA RUTO NA SANG YAANZA KUSIKILIZWA HUKO THE HAGUE





International Criminal Court (ICC) in The Hague, Netherlands

Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto na mwandishi wa habari wa redio Joshua Arap Sang walikana kuwa na hatia katika kusababisha vurugu za baada ya uchaguzi zilizosababisha mauaji miaka mitano iliyopita nchini Kenya wakati wa kuanza kusikilizwa kwa kesi yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) Jumanne (tarehe 10 Septemba).
Jaji wa ICC Chile Eboe-Osuji

Jaji wa ICC Chile Eboe-Osuji aliwataka Ruto na Sang kwa kila moja kujibu mashtaka ya makosa matatu ya uhalifu dhidi ya ubinadamu -- mauaji, kufukuza na mateso -- kwa uwajibikaji wao katika vurugu za baada ya uchaguzi ambazo zilikumba Kenya kufuatia uchaguzi wa 2007."Hatuna hatia," wanaume wote wawili walimwambia jaji.

MAKAMU WA RAIS WA KENYA WILLIAM RUTO

  "Bw. Ruto, kama mwanasiasa mwenye nguvu" alipanga uhalifu "kukidhi kiu yake ya kupata madaraka ya kisiasa", mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda aliiambia mahakama kwa mujibu wa AFP.




"Ni vigumu kufikiria mateso na vitisho ambavyo wakina baba, wakina mama na watoto walikutana navyo ambao walichomwa wakiwa hai, waliteswa hadi kufa au kufukuzwa majumbani kwao," alisema. "Bw. William Ruto na Bw. Joshua Arap Sang ndio wahusika wakubwa katika uhalifu huo."




Sang anatuhumiwa katika kuchochea na kusaidia kuratibu mashambulio -- ikiwa ni pamoja na kudaiwa kutangaza ujumbe wa siri kupitia redio -- dhidi ya mahisimu wa kisiasa na kikabila.

Mashtaka yamekuja siku kadhaa baada ya watunga sheria wa Kenya kupiga kura ya kuidhinisha mjadala wa kujitoa katika utambuzi wa mamlaka ya mahakama hiyo .

No comments:

Post a Comment