Shambulio hilo ni la
pili kufanyika kwenye maeneo mawili tofauti ndani ya saa 24, baada ya lingine
lililofanyika kwenye Mji wa Wajir, muda mfupi baada ya taarifa za kudhibitiwa
kwa watu wanaodhaniwa kuwa magaidi walioshambulia jengo la kibiashara la
Westgate mjini Nairobi.
Serikali ya Kenya
imeliomba Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) kumkamata Mwingereza
Samantha Lewthwaite (pichani), taarifa zinadai kuwa mwanamke huyo alipitia
mpaka wa Namanga, Arusha kwenda Nairobi ambako anahusishwa na tukio la ugaidi.Lewthwaite,
ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Mjane mweupe’ inaaminika anashirikiana na kundi
la magaidi la Al-Shabab la Somalia.
Kundi hilo ndilo
linaaminika lilihusika na mashambulizi kwenye jengo la Westgate jijini Nairobi,
wikiendi iliyopita.Hata hivyo, taarifa ya Interpol ilisema kuwa alikuwa
anatakiwa kujibu mashtaka ya kumiliki mabomu na kupanga njama za ugaidi Desemba
2011.
Interpol haikuhusisha
maombi hayo ya Serikali ya Kenya na mashambulizi ya Nairobi.Pia Lewthwaite
inasemekana aliingia nchini humo kwa kutumia mpaka wa Tanzania.
Baadhi ya vyombo vya
habari vya Afrika ya Kusini, vinasema mwanamke huyo alitumia pasi ya kusafiri
ya nchi hiyo kuingia Kenya kwa kutumia mpaka wa Namanga uliopo mkoani Arusha.
Taarifa hizo zinasema
mwanamke huyo alitumia mpaka wa Lunga Lunga na Namanga kati ya Februari na
Agosti mwaka 2011 akitumia jina la Webb.Habari hizo zinaeleza kuwa, awali
mwanamke huyo alikuwa anaishi Afrika Kusini ambako aliweza kukopeshwa fedha
benki na kuweza kupanga sehemu ya kuishi.
Wakati huohuo, watu
wanaodhaniwa kuwa magaidi wamefanya shambulio kwenye Kituo cha Polisi mjini
Mandera na kuua askari wawili, kujeruhi watatu kisha kuchoma zaidi ya magari 11
jana asubuhi.
Shambulio hilo ni la
pili kufanyika kwenye maeneo mawili tofauti ndani ya saa 24, baada ya lingine
lililofanyika kwenye Mji wa Wajir, muda mfupi baada ya taarifa za kudhibitiwa
kwa watu wanaodhaniwa kuwa magaidi walioshambulia jengo la kibiashara la
Westgate mjini Nairobi.
Shambulio hilo
limefanyika wakati kikosi maalumu cha wataalamu wa mabaki ya mabomu wa Kenya na
wale wa kimataifa kikianza kufanya upekuzi wa jengo hilo, ili kubaini wahusika
halisi wa shambulio hilo na aina ya silaha zilizotumiwa.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment