Thursday, September 12, 2013

KUTANA NA SAMAKI ANAYE TUMIKA KAMA DAWA KANDA YA ZIWA

Dkt. Ngwatya mganga wa jadi na miti shamba aliyerithishwa tangu mwaka 1984 akiwa na umri wa miaka 25-30, mkononi akiwa ameshika samaki wa dawa aitwaye 'Shilonge'.
 Licha ya Ziwa Victoria kutumika kama moja ya njia za usafiri kupitia vyombo vya usafiri majini, kuzalisha samaki watamu aina kwa aina huku maji yake yakitumika kama lishe kwa wanyama (akiwemo binadamu),  mimea na huduma kwa viwanda.

Kuna samaki aitwaye 'Shilonge' hili ni jina toka kwa watu kabila la Wasukuma (Sukuma) samaki ambaye hutumika si kwa chakula bali kama dawa.

Sifa kuu ya samaki huyu (Shilonge) ni kuwa hakai tumboni ni sumu kwa samaki wengine, akiliwa na samaki anatoka mzima mzima kama alivyo hivyo samaki wengi wanaokula samaki wenzao kama vile Sangara humkwepa samaki huyu.

Ili atumike kama dawa, samaki huyu hukaushwa juani kisha husagwa na kuwa kwenye form ya unga, ambao ndiyo dawa akinywa mtu anasafisha tumbo na kuondoa sumu nyinginezo mwilini. (Zaidi Bofya Play kusikiliza)

Samaki Shilonge kwa ukaribu zaidi...

Dawa nyingine zinazouzwa hapa kwa mujibu wa Dkt. Ngwatya anasema kuwa ni pamoja na dawa ya kuvuta bahati iitwayo 'Samba', dawa za kumvuta mpenzi, kuvimba miguu, chango la uzazi, pumu na kadhalika na kadhalika......

Chachandu. na bangili..

Nilikutana na mdau huyu katika mnada wa kata ya Lugeye wilayani Magu mkoani Mwanza kama vipi mzukie upate ukitakacho...Umefuraaaaaaahi mwenyewe..TAARIFA HII NI KWA HISANI KUBWA NA G SENGO, ALIYEKO MWANZA.

No comments:

Post a Comment