Ukiangalia kwa makini
huwezi elewa nini nakuonesha kupitia picha hii, lakini tambua tu ya kwamba tumo
katika wiki ya nenda kwa usalama barabarani,picha hii inakuja siku moja tu
baada ya kamati ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Dar-es-Salaam kuizindua
ikibeba kauli mbiu inayosema! USALAMA
BARABARANI UNAANZA NA MIMI,WEWE NA SISI SOTE.
Mwenye baiskeli hii
naamini ushang’amua ni mtu wa hali gani! Basi alikutwa akitembea kulia mwa
barabara ya Morogoro eneo la Kibanda cha Mkaa, sababu sijui, lori likaja lika
overtake upande huo huo, na kumpiga ndugu huyu! Kisha kumpitia na lori
likasepa! Ila marehemu alionekana maeneo ya mbezi mwisho majira ya saa sita
usiku kwa wauza kahawa.
Jamaa huyu wa boda boda
ambaye jina lake halikupatikana mara moja, yeye alikutana na marehemu eneo la
mbezi mwisho majira ya saa sita usiku, dereva huyo alikua akinywa kahawa,
wakaongea kidogo na kumpa mia mbili na kisha wagaagana alfajiri akapata habari
kuna ajali, kwenda kuangalia ni Yule jamaa,simanzi kubwa.
Askari huyu alifika
eneo la tukio mnamo saa kumi unusu alfajiri,raia wakimtazama mtu huyo walau kama wanaweza kumtambua.
Niwie radhi mtazamji picha hii si nzuri sana, sikua na namna, nilitamani
kumuona dereva aliyemgonga mtu huyu akiwa eneo la tukio kwa kujali tu! Lakini alikimbia!
Na kumuacha mtu huyu akiadhirika hivi! Pole kaka na familia yake pia.
Baiskeli ikawa ipo tu, inapigwa huku na kule na magari yaso na taarifa za tukio lililoko mbele yao.
Japokua kulikua na alama hii, lakini magari yalikua yanajiachia mno! hakika siku yangu ilianza kwa mimi kukumbana na tukio hili la kusikitisha na kunifanya nitetemeke kwa hofu ya nlichoona mbele yangu! EEM MUNGU UTUNUSURU, NA ROHO ZA AJALI NA PEPO WA KIFO NA MAUTI.
No comments:
Post a Comment