Thursday, September 5, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA BENKI MPYA YA UBL JIJINI DAR ES SALAAM 4/9/2013.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua Benki mpya ya UBL, iliyopo Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Sept 4, 2013. Kushoto na kulia kwa Makamu wa ni baadhi ya viongozi wa juu wa benki hiyo, Anwar Pervez na Atif Bakhari.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na viongozi wa Benki mpya ya UBL, kufurahia uzinduzi wa benki hiyo iliyopo Mtaa wa samora jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika leo Sept 4, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa benki ya UBL iliyozinduliwa leo Sept 4, 2013 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBL, Zamees Ghudrey, akizungumza wakati akitoa shukrani baada ya uzinduzi huo.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa benki hiyo, wakimsikiliza Makamu wa Rais , wakati alipokuwa akiwahutubia .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata Keki maalum iliyoandaliwa kuashiria uzinduzi wa benki hiyo mpya ya UBL, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika  Sept 4, 2013.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki mpya ya UBL.
 

No comments:

Post a Comment