Elizabeth Mwase Programu Manager wa Mtandao wa
Watoto na Vijana kutoka Imani Mbalimbali (GNRC) akimpokea Mzee Ali
Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa awamu ya pili ambaye alikuwa mgeni rasmi
ya Siku ya Kimataifa ya Amani iliyoadhimishwa mwishoni mwa Juma jijini
Dar es Salaam ukumbi wa Don Bosco.
Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akisalimiana na baadhi ya
mabalozi na wawakilishi wa jumuiya za maendeleo za nchi wa hisani
wakati wa maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji
Ali Hassan Mwinyi akipokea mfano wa ndege wa Amani kutoka kwa
wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakati wa
maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani duniani jijini
Dar.
Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akihutubia wageni waalikwa
(Hawapo pichani) wakati wa sherehe za Siku ya Kimataifa ya Amani leo
asubuhi jijini Dar. Kulia ni balozi wa Rwanda nchini Ben Rugangazi na
kushoto kwa mgeni rasmi ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
la kuhudumia Watoto (UNICEF) Jama Gulaid.
Meza kuu.
Baadhi ya wanafunzi wa sekondari mbalimbali za
jijini wakitumbuiza kwa nyimbo mbalimbali zenye ujumbe wa kudumisha
Amani na upendo duniani.
Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya mabalozi na wawakilishi wa ofisi za mabalozi
waliohudhuria sherehe hizo kwenye ukumbi wa Don
Bosco.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe
hizo.
.awaasa vijana kutotumiwa na wanasiasa kwa maslahi
yao
.ashangaa wajuzi walivyompachika jina la Ruksa enzi
za miaka 1990s
Na.Mo Blog Team
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan
Mwinyi amesema kuna baadhi ya watu katika jamii hutumia elimu, ujuzi
na maarifa yao kuangamiza, kubomoa na kudumaza Ustawi wa Jamii kwa
maslahi binafsi na si ya Umma. Mo blog inaripoti.
Mzee mwinyi amesema hayo wakati wa kuadhimisha siku
ya Kimataifa ya Amani Duniani inayoadhimishwa 21th Septemba kila mwaka
ambayo imefanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam,
amesema kuna baadhi ya watu wanatumia elimu yao vibaya kwa kupanga
kuua watu wengine kwa maslahi yao aidha ya kisiasa au ya
kiuchumi.
“Elimu kwa kawaida kuleta matokeo mazuri kwa jamii
husika endapo itatumika sawia kwa malengo yaliyokusudiwa na kwa
maendeleo endelevu ya taifa kwa ujumla, ila kuna baadhi ya wanajamii
kutumia ujuzi huu vibaya na kuangamiza ustawi wa jamii husika,”
amesema.
Mzee Mwinyi aliendelea kusema kwamba katika
kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani duniani yenye kauli mbiu
“Education for Peace” ni lazima elimu kwa ajili ya amani iwe endelevu
hapa duniani ili iweze kuleta suluhu na utengamano katika jamii na
mataifa yote duniani.
Amesema kwamba vijana nchini lazima waepuke kutumiwa
na wanasiasa kwa maslahi yao ya kisiasa na wajifunze kutatua matatizo
yao kwa njia ya amani bila ya kuwa na mihemko, jazba, misongo na
hasira ili kuendelea kudumisha amani na upendo katika nchi yetu ambayo
ni kisiwa cha amani.
“nawaasa vijana wakitanzania wa leo hata kama
mmenyimwa haki zenu ni bora kutumia njia ya kistaarabu na kutumia
elimu mnayopata mashuleni bila kusahau macho, masikio na vipawa vyenu
mlivyopewa na mwenyezi mungu katika kutafuta haki yenu kwa njia ya
amani bila misukosuko,” aliongeza.
Mzee Mwinyi alitumia nafasi hiyo kuwashangaa baadhi
ya watu kwa kutumia ujuzi na elimu yao kwa kumpachika jina la Ruksa
bila yeye kujua wametumia muktha gani kumpa jina hilo, lakini Mzee
Mwinyi alitumia jukwaa hilo pia kuwapa ruksa vijana kutumia elimu yao
kuleta hali ya amani na utulivu ndani ya nchi.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Jama Gulaid amesema kwamba Umoja
wa Mataifa uliweka maazimio siku ya kimataifa ya amani duniani ili
watu wanaogombana na kupigana kwa shida mbalimbali kupata nafasi ya
kuweka silaha zao chini katika siku hii adhimu.
Amesema kupitia azimio hilo ambalo lilizinduliwa
mwaka 1982 kwa mara kwanza linatambua uwepo wa watu wanaoathirika na
vita katika sehemu mbalimbali duniani na waliokwishapoteza maisha
kutokana na matatizo vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Naye Mratibu na Mtathimini wa Mtandao wa watoto na
vijana kutoka Imani Mbalimbali (GNRC) Bi, Joyce Mdachi amesema swala
la amani na utulivu linaanzia kwenye kaya hadi ngazi ya taifa kwahiyo
ni muhimu kwa jamii na vijana kuelewa amani inaanzia
nyumbani.
“jamii iliyolelewa katika mazingira mazuri ina nafasi
kubwa ya kuleta matokeo chanya kwenye mustakabali wa taifa kwa ujumla
lakini jamii iliyolelewa vibaya haiwezi kubadilisha taifa kwa sababu
ni zao la tunda baya,” alisema.
Mdachi alisisitiza kwamba kuporomoka kwa maadili
ndani ya jamii ya leo swala hilo pia lilianzia kwenye kaya ya mtu
mmoja mmoja hadi ngazi ya taifa ambapo leo hii taifa linashuhudia
mambo ya kifisadi, rushwa na ubadhilifu wa mali za umma kunakofanywa
na viongozi waandamizi.
No comments:
Post a Comment