Monday, September 9, 2013

IRINGA KULINOGA!!!!! TWENZETU DODOMA NA MOROGORO

 sehemu ya meza kuu. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS,Salim Abri  akizungumza na wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye semina ya kamata fursa twenzetu,ASAS amejitolea kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kusaidia vikundi vitakavyoamua kutumia fursa ya kulima vitunguu na kuendelea kuwa wajasiliamali katika fursa mbalimbali. 
  Mfanyabiashara mkubwa wa mjini Iringa,Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS,Salim Abri  akionesha baadhi ya fursa zilizopo mkoani Iringa kwa kuonesha kitunguu cheupe kama moja ya bidhaa za thamani zinazopatikana mkoani humo,ASAS ameeleza kuwa vitunguu hivyo vinauzwa kwa kilo kwenye SuperMarket nyingi,anasema kuwa vitunguu hivyo vinadaiwa kutoka nje ya nchi,lakini vitunguu hivi inawezekana kuvipanda hapa mkoani Iringa na vijana wakanufaika kupitia mradi wa vitunguu hivyo.
 Mdau mkubwa wa michezo nchini Fredrick Mwakalebela naye alipata wasaa wa kuzungumza na wakazi wa Iringa na kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwawezesha wakazi wa mkoa huo watakaoweza kutumia fursa ya rasilimali zilizopo mkoani hapo.
Msanii wa kughani mashairi Mrisho Mpoto, akizungumza na wakazi wa Iringa waliojitokeza kusikiliza mafunzo ya namna ya kujikwamua kimaisha kwa kutumia fursa kwa rasilimali zilizopo mjini Iringa.
 Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Iringa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mtakatifu Dominic  mjini Iringa,ambapo watu mbalimbali wamepata fursa ya kujua namna ya kutumia sasilimali zilizopo mkoni humo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.
 Mwakilishi kutoka NSSF Makao Makuu Salim Khalfan, akizungumzia Fursa kwa upande wa NSSF wanavyoweza kuitumia wakazi wa Iringa katika kupata mikopo itakayowawezesha kujikwamua kimaisha.
 Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akihitimisha semina ya Kamata fursa twenzetu mepema leo mchana ndani ya mkoa wa Iringa.
 Baadhi ya Wadau mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwey´nye Semina ya kamata fursa kwa vijana twenzetu. 
 Wanafuatilia. 

 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Nick wa pili akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Iringa ,namna ya kutumia fursa zilizopo mkoani hamu kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.
 Bwana Shamba Yona Daniel akizungumza na wakazi wa Iringa tayari kwa kuwaonyesha namna ya kutumia Fursa kupitia kilimo.
 Wakifuatilia mada mbalilmbali ndani ya semina hiyo. 
 Meneja wa Mkoa wa Iringa kutoka taasisi ya PSI-Tanzania,Rogers Ari akizungumza fursa mbalimbali kwa vijana ikiwemo na suala zima la kujilinda kiafya  kwa namna yoyote ile,ili kuwa fiti katika suala zima la kuzitumia fursa wanazokumbana.

No comments:

Post a Comment