Rastafarians nchini Malawi wameonesha nguvu yao kwa pamoja baada
ya kuungana katika maandamano ili kuisukuma serikali ya nchi yao ili waondoe
katazo waliloliweka dhidi ya watoto wa kirasta wasihudhurie masomo wakiwa na
nywele zao zilizosokotwa ,wao wanadai kua katazo hilo halimo katika katiba ya
nchi yao kuwakataza watoto wao na kuwazuilia elimu ati tu kwasababu tu ya imani
yao ambayo inawataka kuwa katika mtazamo huo wa nywele.
Pamoja na kutokuweko
kwa sheria inayokataza nywele ndefu na mtazamo wan chi ya Malawi, maRastafarians
hao kutoka kusini wa Africa walizuiliwa kwa kipindi kireefu kuto wasiende
katika shule za umma wakiwa katika hali hiyo ya kuwa na dred locks, na ikiwa
mtoto atakwenda shule nazo basi atatakiwa kunyoa ama azuiliwe kuingia shule
Lakini raisi wa umoja
wa ki Rastafari, Ras Judah I,ameeleza kua dreadlocks ni moja ya utambulisho ama alama katika
imani yao ,na kusema kwama zuio hilo ni
sawa na kuwanyanyasa wanafunzi na kuvunja haki za msingi za mwanafunzi na pia
uhuru wa kuabudu vitu ambavyo vyote havimo katika katiba ya nchi Malawi.
Na rais huyo amesema
kwamba wanasubiri muitikio wa serikali yao, kama hawatajibu lolote, hatua
inayofuata ni kupeleka muswada na madai yao katika ofisi ya raisin a bunge pia1
na wakijibu pia wataangalia hatua ya kuchukua.
No comments:
Post a Comment