Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta alitangaza Jumanne jioni (tarehe 24 Septemba) kuwa kuzingirwa huko
kumemalizika, lakini maafa yalikuwa "makubwa" huku watu wasiopungua
67 walikufa, pamoja na watu watatu kutoka kikosi cha usalama.
Alisema kuwa
washambulizi watano waliuawa na kuwa washukiwa 11 wamekamatwa.Lakini Jumatatu
jioni, wizara ya mambo ya ndani ilitangaza kuwa kuzingirwa huko kuliisha.
"Tunadhibiti
Westgate," wizara hiyo ilisema kupitia Twitter, saa 60 baada ya wanamgambo
wa al-Shabaab kuvamia jengo hilo.Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani alisema
mateka wote inaaminika waliokolewa.
"Vikosi vyetu
maalumu viko ndani ya jengo vikikagua vyumba. Tunafikiri kuwa kila mtu, mateka,
wameondoka, lakini hatutaki kutumia fursa zozote," Manoah Esipisu
aliiambia AFP.
"Vikosi maalumu
viliita jambo hili kuwa ni usafishaji. Wakati huu ambao hawajakutana na
pingamizi yoyote, lakini bila shaka hatupuuzilii uwezekano kwamba kuna baadhi
wanaweza kuwa wamejificha katika maeneo ya mbali au kwenye kona,"
aliongezea.Usiku wote eneo la karibu na kituo hicho cha biashara lilikuwa
kimya, pamoja na watumishi wa usalama wakionekana kupumzika.
Milio ya bunduki ya
hapa na pale katika eneo la biashara iliibuka tena Jumanne asubuhi (tarehe 24
Septemba), saa chache baada ya maofisa kudai kuwa vikosi vya Kenya vilikuwa
"katika udhibiti" wa al-Shabaab wa eneo la soko hilo la biashara la
kitajiri -- na al-Shabaab ilidai bado inawashakilia mateka.
Hakuna taarifa
zilizotolewa kuhusu idadi ya mateka walioachiwa, au ambao bado wanashikiliwa,
lakini watu 63 walirekodiwa mapema kutoonekana na Shirika la Msalaba Mwekundu
la Kenya, idadi hiyo inajumuisha mateka pamoja na wengine ambao wanaweza kuwa
waliuawa.
"Mateka ambao
walikuwa wanashikiliwa na wajahidina hao ndani ya Westgate bado wako hai,
wakionekana kuudhika sana, lakini, hata hivyo hai," al-Shabaab ilisema
katika ujumbe uliotumwa katika akaunti yao ya sasa ya Twitter.
Mfululizo wa akaunti za
Twitter zinazoendeshwa na wanamagambo hao walio shirika na al-Qaeda zilifungwa
kutoka shambulio hilo lililpoanza, lakini wamefanya haraka kufungua akaunti
mpya.
Pia Jumanne asubuhi,
polisi wa Kenya walisema walikuwa wanategua vitu vyenye milipuko vilivyowekwa
na wanamgambo katika duka hilo kuu."Tunaondoa vifaa vya milipuko ambayo
ilikuwa vimewekwa na magaidi," polisi wa Kenya walisema katika ujumbe wa
Twitter.
Hakuna maelezo
yaliyotolewa kuhusu aina na ukubwa wa milipuko, lakini yanaongeza kipengele cha
ziada cha hatari katika kuzingira, na kuibua maswali kuhusu ni jinsi gani
viongozi wa Kenya "wanaidhibiti" hali hiyo.
Majibu ya serikali
yakosolewa
Mshauri wa usalama
anayekaa Nairobi Moses Omusula alisema serikali ya Kenya inapaswa kuwa na
ulinganifu zaidi katika taarifa inazozitoa kwa umma.
"Nchi inaelewa
kwamba hali ya mateka na ugaidi ni dhana mpya nchini Kenya. Wananchi pia
wanaelewa kwamba baadhi ya taarifa zinaweza kuwa nyeti, lakini itakuwa vizuri
kwa serikali kuwa na mambo yanayolingana," aliiambia Sabahi.
Omusula alisema umma
utapoteza uaminifu kwa serikali kama taarifa zinazotolewa haziendani na
uhalisia.Alisema umma, na hasa familia za mateka, zinataka taarifa sahihi ili
kufanya uamuzi thabiti.
Simiyu Werunga, kapteni
mstaafu wa jeshi la Kenya, alisema mwitikio wa vikosi vya usalama vya Kenya
katika kuzingira Westgate ulianza kwa nguvu, lakini ulipungua kadri hali
ilivyoendelea.
"Maofisa walikuwa
na ujasiri siku ya kwanza tukio lilipoanza, lakini mapigano hayo ambayo
yalikusudia kuliokoa jengo zima yalisimama kabisa tangu hapo, na kumekuwa na
matamko isiyo sambamba kuhusu mafanikio yao," Simiyu, ambaye pia ni
mkurugenzi wa Kituo cha Afrika cha Usalama na Masomo ya Kimkakati, aliiambia
Sabahi.
"Tumewasikia
wakitamka kwamba wamechukua udhibiti, wakati kinyume chake bado tunasikia milio
ya risasi na matamko mengine kwamba bado wanasafisha eneo," alisema.
Alisema ulikuwa ni
uchungu kwa vikosi vya usalama kuripoti kwamba wamelichukua jengo na kuwaokoa
mateka wote, wakati familia bado zinaripoti watu waliopotea ambao ama bado
wanashikiliwa kama mateka au wameuawa.
Simiyu alisema
kushindwa kwa vikosi vya usalama kuwa na chanzo kimoja cha taarifa
kinacholingana kulikuwa kunasababisha mawasiliano duni na utatizaji.
"Wanapaswa kuwa na
chanzo kimoja cha mawasiliano, sio waziri wa usalama wa ndani, mkuu wa Vikosi
vya Ulinzi Kenya na inspekta jenerali kila mmoja akizungumza kivyao,"
alisema. "Na kwa wananchi, mambo yatakwisha watakapowaona viongozi
waandamizi wa serikali wakitembelea jengo ili wao waamini kwamba jengo
limekombolewa.
Kufanya mambo mbaya
zaidi, wakati wanafamilia ya waliopotea, waandishi wa habari na watazamaji
wengine waliokusanyika Jumanne karibu na Westgate wakitafuta majibu, au kwa
kudadisi tu, polisi wa Kenya walitawanya makundi ya watu kwa gesi ya kutoa
machozi.
UMOJA WA AFRIKA
WADHAMIRI KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA AL-SHABAAB
Al-Shabaab siku ya
Jumanne ilionya itafuatilia uzingiraji unaoendelea katika eneo la maduka la
Westgate pamoja na mashambulizi zaidi kama vikosi vya Kenya havitaondoka mara
moja Somalia.
"Kama haitaondoka,
jua kwamba hiyo ni sehemu tu ya tutakachokifanya... mtarajie siku mbaya,"
msemaji wa al-Shabaab Ali Mohamud Rage alisema kwa Kiarabu katika matangazo ya
redio yaliyotolewa na wenye msimamo mkali.
Lakini Umoja wa Afrika,
ambao chini yake vikosi vya Kenya vinapambana na al-Shabaab nchini Somalia,
umedhamiria kuongeza nguvu."Dhamira yetu ni kupambana zaidi sasa kuliko
ilivyowahi kutokea," naibu wa mkuu wa tawi la utendaji la Umoja wa Afrika,
Erastus Mwencha, aliiambia AFP.
Mwencha alisema
umwagaji wa damu umeonyesha wazi ugumu wa kupambana na waasi wa al-Shabaab,
ambao vitisho vyao vinaendelea nje ya mipaka ya Somalia.
"Hili ni lengo
linalosonga [ambapo] tunatakiwa kujisasisha sisi wenyewe na kuendelea kuwa
macho katika mapigano yetu," alisema, akiongeza kwamba jumuiya ya
kimataifa lazima ishirikiane kubadilisha intelijensia na wataalamu ili kuondoa
vitisho vya al-Shabaab.
Al-Shabaab walisema
shambulio la maduka makubwa lilikuwa katika kulipiza kisasi kwa jeshi la Kenya
kuiingilia nchi ya Somalia, ambako kulianza karibia miaka miwili iliyopita.
Wanajeshi watatu wa
Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) walithibitishwa kufariki Jumanne, wengine wanane
waliojeruhiwa bado wapo hospitali na baadhi yao wapo katika hali mbaya.Msemaji
wa jeshi Kanali Cyrus Oguna alisema KDF haijazuiliwa kumaliza operesheni huko
Westgate.
"Hali ya ulaini na
ugumu wa maduka makubwa ya operesheni ya uokoaji ya Westgate uliozingirwa
ulihitaji uangalizi mkubwa na tahadhari kuhakikisha ulinzi na usalama wa wahudumu,"
alisema Oguna katika tamko lake kwa gazeti la The Standard la Kenya. "KDF
ilifikia dhamira hii kwa kiwango cha hali ya juu cha utaalamu."
Hospitali za Nairobi
zabeba mzigo wa shambulio la kigaidi lililotokea katika maduka makubwa ya
WestgateHospitali kubwa mbili za Nairobi, Aga Khan na MP Shah, zimebeba jukumu
la kuwahudumia majeruhi na waathirika na walishtushwa na shambulio la Westgate.
Hospitali hizo mbili za
binafsi, zilizopo karibu na kituo hicho cha ununuzi, ziliwahudumia zaidi ya
wagonjwa 200 ambao walikimbizwa hapo kwa dazeni za magari ya kubebea wagonjwa
ya binafsi na ya serikali.
"Hadi Jumapili
tulikuwa tumepokea wagonjwa 129. Kati yao tuliwalaza wagonjwa 43 na wengine
walitibiwa na kuruhusiwa," Mwenyekiti wa Hospitali ya MP Shah Hospital
Manoj Shah aliiambia Sabahi.
"Tulipopokea
habari hizo za kuhuzunisha kuhusu shambulio hilo, uongozi wa hospitali
ulikusanya wataalamu na tulikuwa na jopo la madaktari 40 na waliojitolea zaidi
ya 100 ambao huduma yao ilikuwa muhimu katika kupokea majeruhi na kuwasukuma
kwa kutumia vitanda vya wagonjwa kuelekea katika vitengo mbalimbali vya
matibabu,"alisema.
Shah alisema hospitali
ilipokea wagonjwa 133, lakini 27 walikufa wakati wakipata matibabu.
"Polisi na Chama cha Msalaba Mwekundu wanafanya kazi nzuri ya kutusaidia
kubainisha baadhi ya taarifa za waliofariki na kuwasiliana na watu wao wa
karibu," alisema.
Hospitali ya Aga Khan
ilipokea watu 60 kutoka katika tukio la kisikitisha la Westgate, pamoja na
wengine watatu wanaougulia majeraha yao, kwa mujibu wa ofisa uhusiano wa
hospitali hiyo Eunice Mwangi.
Hospitali hizo zimefuta
malipo ya kabla ya kutibiwa na zinatoa matibabu bure kwa waathirika wote,
Katibu Mkuu wa Msalaba Mwekundu wa Kenya Abbas Gullet aliiambia Sabahi.
"Wengi wa majeruhi
ambao tunawapokea wamevunjika miguu, wana majeraha ya risasi, majeraha ya
mabomu, viungo vilivyopishana na michubuko midogo na mikubwa," Neeraj
Krishnan, daktari wa upasuaji wa mifupa katika Hospitali ya MP Shah, aliiambia
Sabahi.
Ingawa anaelewa
itachukua miezi sita au zaidi kwa yeye kutembea tena kwa miguu yake ambayo
ilipigwa risasi nyingi, Edwin Njoroge, wakala wa kuuza bima, mwenye umri wa
miaka 35, alikuwa amepeleka stika ya bima kwa mteja katika maduka makubwa ya
Westgate, anaamini shambulio halitafifisha moyo wake.
"Ndiyo, miguu
yangu yote miwili imevunjika lakini moyo wangu haujavunjika. Kwa kuwa ugaidi
huu wa kikatili haukuchukua maisha yangu, siwezi kutembea tu lakini
sijakatishwa tamaa ya kuwa wakala wa bima. Nitatembea kwa miguu yangu siku
chache zijazo," alisema Njoroge akitabasamu pamoja na maumivu makali
aliyokuwa akiyapata katika Hospitali ya MP Shah.
Mgonjwa mwingine, Popat
Singh, mwenye umri wa miaka 48 alikuwa amemshukisha tu mkewe katika maduka hayo
makubwa kwa ajili ya kufanya baadhi ya ununuzi, na alikuwa katika gari lake
akisoma gazeti wakati mshambuliaji alipompiga risasi.
"Walinipiga risasi
katika kiwiko cha mkono wangu wa kulia na sijawahi kupata maumivu makali kama
niliyoyapata," alisema Singh. "Lakini nilikwepa kabla ya risasi ya
pili. Watu hawa ni waoga…nitarejea mtindo wangu wa maisha katika maduka makubwa
ya Westgate wakati mkono wangu utakapopona kwa sababu kuacha maana yake ni
kuwatia moyo magaidi."
No comments:
Post a Comment