Mwimbaji wa nyimbo za
Injili Jijini Nairobi,Kenya,George Barasa maarufu kama Joji Baro amejiatangaza
kuwa yeye ni shoga.Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 22 akizungumza na mtandao
mmoja wa nchini humo alisema kuwa alizaliwa Jijini Nairobi na baadaye kuhamia
Bungoma miaka michache baadaye.
Hapa alipokuwa yupo shule.
Alipokuwa anasoma shule
ya Mtakatifu Paulo Miluki High School ndipo alipoanza kujifunza vitendo hivyo
vya ushoga na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kiongozi mmoja wa kanisa
Katoliki.
Aidha ameongeza kuwa
pamoja ya kuwa ni shoga pia ameathirika na ugonjwa hatari wa Ukimwi pia ni
mwanaharakati wa kutetea Haki za Mashoga na Wasagaji na wana zaidi ya wanachama
2,800,Ambao wote ni mashoga na wasagaji ambapo vijana idadi yao 15 na watu
wazima ni 68.
Alisema kuwa aliamua
kuhamia Mjini EMBAKASI BAADA YA FAMILIA yake kumtenga alipojuliakana
anajihusisha na vitendo hivyo.
Machi 11, 2012 ,
Madaktari walimpima na kugundulika kuwa ni mwathirika wa VVU / UKIMWI na kwamba
amedai kuwa kwenye muziki wa INJILI amekuwa akipata upinzani mkubwa kutoka kwa
wanamuziki mwenzake wa muziki huo.
Anasema amechoka
kuhukumiwa na kuonewa huku akinyanyapaliwa na watu wengine baada ya kugundulika
kuwa nafanya vitendo hivyo.
‘Mimi ni binadamu,Kama
binadamu yeyote naumia sana ninavyonyanyapaliwa,’alisema Barasa.Anasema kwenye
masuala ya urembo hayuko nyuma ana mawigi 15 na zaidi ya pea za viatu virefu
‘High hills’30.
‘Napenda sana urembo na
pia naandika kitabu cha maisha yangu kiitwacho "Dream Boy"ambacho kitaeleza
historia nzima ya maisha yangu na jina la albanu yangua ya injili inaitwa
"Bora Siku"alisema Barasa.
ee mungu tuonee huruma maana hatujui tutendalo
ReplyDelete