Thursday, September 19, 2013

WENZIWE WAMESHINDWA NINI? YEYE SIRI YAKE NINI? SIJABAINI BADO



Maashallah motto ana mvuto wa hatari, japokua ananyanyua vitu vizito, kinachonishangaza, huko huko aliko, wenziwe wakinyanyua vitu vizito wanashupaaje? Songa nayo!

Yuko vizuri mno! Eeeeh, namsifia motto wa kike mwenzangu, yes kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo!
Hapa akiwa na nguo za mazoezi na tabasamu tele usoni
Jane akiwa kwenye push ups! Uso nyororo, anayafurahia mazoezi, jamani nambieni huyu ameweza ana nini wenziwe wawe wameshupaa sababu ya stereoid? Midawa yao hiyo, sijui nimepatia? Ah humo humo.
 Mdada huyu Lisa Cross,ana miaka 35 leo na anadai kua mazoezi ya kuinua vitu vizito yamemsaidia sana kutoka katika ugonjwa uliokua ukimsumbua, na hayo aliyamudu baada ya kua na boyfriend mnyanyua vitu vizito,mwanzoni alikua mwembamba mno,na babake alimpiga picha, leo ana kula calorie 5,000 katika milo midogo kumi anajisikia furaha kwa muonekano wake.
Ms Lisa Cross ndivyo alivyokua awali, na picha hii aliipiga babake.back to Jane!
jane akikubadilishiamikao na nguo tofauti tofauti, anajivunia muonekano wake na kwa hakika hatishi kama wengine walivyo.
Huu ni muonekano wake kwa nyuma, ameondoa mafuta mwilini, na anaonekana vyema tu! Kwakweli namtamani,ningekua mimi lol! Kiukweli stanii.

Wanyanyua vitu vizito walio wengi huwa wana finyangika na kua na miili ilo shupaa, lakini kwa mdada huyu kutoka East Africa ,aliyezaliwa na kukulia katika jiji la Nairobi nchini Kenya,aitwaye  Jane Mukami ana tajwa kama  the sexiest female body builder in Kenya.

Kwa sasa Jane anaishi  Atlanta, na huko  Jane anajulikana kama ’fitkenyangirl’na anashawishiwa kushiriki katika mashindano ya ulimbwende akiwa na muonekano wake huo .

Jane yeye ame  graduate katika Computer Information Systems katika chuo cha Kennesaw State University, Mukami amefundishwa na mwalimu wa kunyanyua vitu vizito  aitwaye Rashid ‘Roc’ Shabazz wa shirikisho la   Roc International Federation of Bodybuilding (IFBB).

Jane Mukami amejaaliwa mafanikio kadhaa maishani  mwake na hasa upande wa body building competition katika jimbo la South Carolina,mnamo mwaka  2011, katika  half marathon imwaka  2009 ambapo alifuzu na kuchukua nafasi ya  1st, na pia katika michuano  body building huko  Atlanta, na hapo alinyakua nafasi ya 2.


No comments:

Post a Comment