Friday, November 30, 2012

VIONGOZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA BARABARA YA ARUSHA-NAMANGA-ATHI RIVER






Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan naye alikuwepo hapo uwanjani.

JENGO LA JUMUIYA YA AFRICA MASHARIKI LAZINDULIWA ARUSHA



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  wakiwa katika chemba ya mikutano ya Bunge la Jumuiya ya Afrika mashariki katika jengo jipya la makao makuu ya Jumuiya 
 VIONGOZI KATIKA PICHA YA PAMOJA.

Tanzia: Zamaradi Mketema wa Clouds Media Group afiwa na mama yake mzazi.



                    Zamaradi Mketema wa Clouds Media Group.

Mtangazaji wa kipindi cha 'Take One' cha Clouds TV Zamaradi Mketema, amefikwa na msiba wa mama yake mzazi, aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa.

mama yake Zamaradi ambaye ni mama yetu pia alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar-Es-Salaam. Kegajo.com inampa pole Zamaradi na ndugu wote, wana Clouds Media Group na marafiki wote kwa msiba huo, R.I.P mammy!!!!

Thursday, November 29, 2012

HII NILIIFANYA ZAMANI SANA, KUANDIKA NAMBA CHINI





hii kali sijui askari huyu alikuwa anachora nini hapo chini hii ni barabara ya mbeya peak kwenda uwanja wa sokoine mbeya

M23 sasa waondoka Goma






M23 wakiondoka Goma


 Kufuatia juhudi za kimataifa na mataifa jirani, hatimaye waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekubali kuondoka Goma na sasa wanakwenda kujikusanya kwenye mji wa Sake, nje kidogo ya Goma.

TUME YA UCHUNGUZI WA AJALI YA BOTI ZANZIBAR WATAKA KUSHTAKIWA KWA MMILIKI WA MELI, MAAFISA WA SERIKALI




Tume moja ya serikali ya Zanzibar imependekeza kushtakiwa kwa mmiliki wa meli na maafisa wote wa bandari waliohusika na ajali ya boti mwezi Julai iliyopoteza maisha ya watu 81 na kusababisha zaidi ya 200 ambao bado hawajapatikana, liliripoti gazeti la Daily News .
"Mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti yanajumuisha hatua za kisheria na kinidhamu dhidi ya wale wote waliotajwa ndani yake," alisema Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar na kiongozi wa tume hiyo, Abdulhakim Ameir Issa. "Tume pia imeishauri serikali kupitia sheria za usalama baharini na kuimarisha idara ya uokozi na udhibiti wa majanga."

PESA ZA KIGENI, UPUNGUFU WA NISHATI VYAYUMBISHA SHILINGI YA TANZANIA



Watu kutoka mji wa Wete Zanzibar wakinunua chakula sokoni. Bei za chakula zilipanda karibuni hadi kufikia asilimia 100 kutokana na kubadilikabadilika kwa bei za fedha za kigeni.
Kubadilikabadilika kukubwa kwa bei za chakula ambako Tanzania imeshuhudia katika miezi ya karibuni ni ishara kwamba uchumi wa nchi haukutengamaa kimuundo, wanauchumi wasema.
Baada ya bei za chakula kushuka kwa muda mfupi kutokana na kukaribia kwa msimu wa mavuno wa mwezi Oktoba, zilipaa tena mwezi wa Novemba baada ya nchi kukumbwa na uhaba wa mafuta.
Kwa mujibu wa data zilizotolewa tarehe 23 Novemba na Wizara ya Viwanda na Biashara, baadhi ya bei za mazao zilipanda hadi kufikia asilimia 100 katika wiki za mwanzo za mwezi huu.
Kwa mfano, mjini Dar es Salaam, bei kwa kila kilo moja ya maharage ilipanda kutoka shilingi 600 (senti 37 za dola) hadi shilingi 1,200 (senti 75 za dola), bei ya mahindi ilipanda kutoka shilingi 600 (senti 37 za dola) hadi shilingi 700 (senti 44 za dola), mchele kutoka shilingi 1,600 (dola 1) hadi shilingi 2,200 (dola 1.37) na unga wa ngano kutoka shilingi 600 (senti 37 za dola ) hadi shilingi 900 (senti 56 za dola).
Ili kujilinda dhidi ya kuanguka kwa bei ya shilingi, Watanzania wengi wanategemea dola ya Marekani na pesa nyengine za kigeni kwa ajilli ya kununua na kuuza bidhaa, utaratibu ambao unazidisha kuiyumbisha pesa ya nchi na kusababisha kupaa kwa bei za chakula, kwa mujibu wa Mushengezi Nyambele, mchumi na katibu wa zamani wa bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.
"Hata watu wa kawaida wamepoteza imani na fedha yetu," aliiambia Sabahi. "Wote wanachagua dola, jambo ambalo husababisha uhaba wa dola nchini, na kwa hivyo kuchochea kuongezeka kwa bei." Alisema kuwa mafuta yanapanda kwa sababu mzunguko mdogo wa dola nchini Tanzania, badala yake kuathiri bei za bidhaa na huduma.

MUENDELEZO WA PICHA ZA MAZIKO YA SHARO MILLIONEA


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole  Zaina Mkieli, Mama wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga.
. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea.

Wednesday, November 28, 2012

SAFARI YA MWISHO YA SHARO MILLIONEA



Jeneza lenye mwili wa Hussein a.k.a Sharo MILLIONEA.
Aliyekua Sharo Millionea akiombewa dua kabla ya maziko.
Ndugu jamaa na marafiki wakishiriki katika duaa hiyo!

MKUTANO UNAENDELEA DOHA

 Bi Fauzia M. Haji, mwenyekiti wa kamati ya wataalam ya mabadiliko ya tabianchi kutoka Ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, akifuatilia mjadala wa wa kundi la Africa katika mkutano wa 18 wa duania wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini Doha leo.
Kushoto Bw. Richard Muyungi Mwenyekiti wa kamati ya dunia ya sayansi na taaluma ya mabadiliko ya tabia nchi akijadili masuala muhimu yatakayojadiliwa katika kilimo na msaidizi wake Bi Hanna Hoffmann ofisini kwake mjini Doha, kabla ya kuendelea kuendesha mikutano ya kamati hiyo inayoendelea katika mkutano wa 18 wa dunia wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi leo.

UJUMBE WA TURKEY WAKUTANA NA WAZIRI WA HABARI MICHEZO ZANZIBAR



Waziri wa Kilimo na Chakula wa Turkey Mchmet Mehdi Eker kulia akiwa pamoja na Balozi wa Turkey nchini Tanzania Ali Davutoglu wakimsikiza Waziri wa Habari Utalii,Utamaduni na Michezo Saidi Ali Mbarouk hayupo pichani walipokua wakibadilishana mawazo kuhusu kuimarisha sekta ya Utalii  Zanzibar huko katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Kikwajuni .
Ujumbe wa Turkey ukiongozwa na Waziri wa Kilimo na Chakula wa Turkey Mchmet Mehdi Eker wakimsikiza kwa makini Waziri wa Habari Utalii,Utamaduni na Michezo Saidi Ali Mbarouk mwenye suti kushoto huko katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Kikwajuni .

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMJULIA HALI SHEIKH MKUU WA BAGAMOYO, ABDALLH MASOUD JEMBE



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Sheikh Mkuu wa Bagamoyo, Sheikh Abdallah Masoud Jembe, anayesumbuliwa na maradhi, wakati Makamu wa Rais alipofika nyumbani kwa Sheikh huyo, eneo la Ramiah mjini Bagamoyo.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA OFISI YA CCM MAKAO MAKUU YA WILAYA YA BAGAMOYO



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mjumbe wa NEC Taifa, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi na wanachama wa CCM, baada ya kuzindua rasmi Ofisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM ya Wilaya ya Bagamoyo.

HILI NDILO GARI ALILOPATA NALO AJALI SHARO MILLIONEA KABLA YA KUTOLEWA ENEO LA TUKIO(PICHA 5)


Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Sguhuda akiangalia gari alokuwemo Sharo ilivyo haribika.

PICHA ZA BALOZI WA CHINA NA WANAHABARI



Balozi wa China nchini Tanzania.

KUMBE MSANII JOHN S. MAGANGA ALIFANYIWA UPASUAJI KIMAKOSA KABLA YA KIFO CHAKE


JOHN S. MAGANGA

 
                              Mwili wa John ukiwa umebebwa na wasanii wenzake.

WADAU WAJITOKEZA KUCHANGIA HARAMBEE YA UJENZI WA MABWENI YA WANAFUNZI ILIYORATIBIWA NA TEA




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka (kulia) akiongozana na mgeni rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasichana, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mstaafu, Dk. Asha Rose Migiro ambapo katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 278 zilipatikana
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dk. Naomi Katunzi akizungumza katika harambee hiyo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA SHULE YA MSINGI YA KIROMO-MJINI BAGAMOYO



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa Shule ya Msingi Kiromo, iliyopo Wilaya ya Bagamoyo-Mkoa wa Pwani, iliyokarabatiwa na Kampuni ya Airtel Tanzania.

Tuesday, November 27, 2012

MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI NAIROBI, KENYA



Mwanasheria wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo. Kushoto ni bwana Wilbert Kawa Katikati ni bwana Dr. Richard Sezibera na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano Uganda. Mkutano huu umefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Kenyetta  jijini Nairobi

WILDAF yaendesha Mkutano kwa Wadau wake wa Kupiga Vita Ukatili Dhidi ya wanawake nchini





Brass Band ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam .



 Washiriki wa Maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.


Moja ya Mabango yenye Ujumbe wa Kupiga Vita Ukatili dhidi ya Wawanake.

SHAROBARO IONE HAPA

R.I.P. Sharomillionea hatunaye tena




                Hussein Ramadhani a.k.a Sharo Milionea
Msanii Maarufu nchini Tanzania aliyekuwa anakuja kwa kasi katika muziki na pia matangazo ya biashara likiwemo la Airtel Money la kampuni ya simu ya Airtel Hussein Ramadhani  aliyejulikana kwa jina la Sharobaro a.k.a Sharo Milionea amefariki dunia

Friday, November 23, 2012

RIHANNA ANATISHA !! AIFIKIA RECORD YA MADONNA, HUENDA AKAMFIKIA MICHAEL JACKSON.



The Diamonds hit maker’ Rihanna anaonekana ataandika vyema tarehe za mwaka huu kwenye diary yake kwa sababu kila kukicha anazidi kufanya makubwa katika career yake na anazidi kuweka historia kwa kufanya hit songs.
‘Diamonds’, wimbo wa kwanza kutoka kwenye album yake ‘Unapologetic’ inatarajia kupanda hadi nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100 ya wiki ijayo, hii itamfanya RiRi awe amefikisha idadi ya nyimbo 12 zilizoshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Hot 100, idadi inayomfanya alingane na mwanamuziki mkongwe Madonna katika historia ya miaka 54 ya chart hiyo.

HAPPYBIRTHDAY DINA MARIOS WA CLOUDS MEDIA GROUP


Happy birthday Dina, all the best and bright future

KATIKA sauti ambazo hurindima na kusikilizwa sana kwenye anga za miji mikubwa ya Tanzania majira ya mchana ni ya Dina Marios, mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds FM.
Ni mwendeshaji wa kipindi cha Leo Tena. Amefanikiwa kujikusanyia mashabiki wengi kutokana na ubunifu na mbwembwe zake.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA, DA-ES-SALAAM.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Brandina Chuwa, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi  wakati wa ufunguzi wa  Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika.Jijini Dar-Es-Salaam.

Mashabiki wa Tottenham washambuliwa Roma




Idara ya polisi mjini Roma imetangaza kwamba mashabiki kadha wa Tottenham wamejeruhiwa, mmoja wao vibaya mno, kufuatia fujo kuzuka katika baa moja.
Kulingana na taarifa katika vyombo vya habari nchini Italia, wapenda soka hao walishambuliwa na mashabiki wa timu ya kandanda ya nyumbani, Lazio, huku pambano likitazamiwa leo usiku kati ya timu hizo mbili.

Mkewe Gbagbo kufikishwa the Haque





 Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Bi Simone, Gbagbo. Bi Gbagbo anasakwa kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kivita wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka baada ya uchaguzi wa urais nchini humo.


Mumewe tayari alishakamatwa na anasubiri kesi yake kuanza katika mahakama hiyo iliyoko The Haque, kuhusiana na madai hayo ya uhalifu wa kivita.Takriban watu 3,000 waliuawa kwenye machafuko yaliyotokea baada ya ya Gbagbokukataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa Urais.

Thursday, November 22, 2012

MAGAZETI YA LEO







Wachezaji 5 watangazwa




Majina ya wachezaji watano wanaowania tuzo la BBC la mchezaji bora zaidi barani Afrika mwaka 2012 yametangazwa.
Yaya Toure, kwa mwaka wa pili mfululizo, yupo kwenye orodha hiyo.
Mwenzake katika timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba pia yumo.

Wachezaji wengine ni pamoja na Demba Ba kutoka Senegal, Younes Belhanda wa Morocco na nahodha wa timu ya Zambia, Christopher Katongo.Huu umekuwa ni mwaka wa ufanisi kwa wachezaji hao, na timu za wachezaji wanne zikionyesha ustadi kwa kupata vikombe.

Inaelekea Drogba aliondoka Chelsea wakati muwafaka, mara tu baada ya timu yake kukamilisha msimu kwa ushindi wa klabu bingwa barani Ulaya, hii ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya klabu, na vile vile akipata bao la ushindi katika fainali ya Kombe la FA.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA INDIA NCHINI



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa India Nchini Tanzania, Dednath Shaw, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo.

Wednesday, November 21, 2012

MAGAZETI YA LEO 21/11/2012


     

      

ASKOFU WA KWANZA MWANAMKE WA KIANGLIKANA





Ellinah Ntombi  Wamukoya ameteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa kike wa kanisa la Kianglikana barani Afrika.Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa, Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi huo heshima kwa kina mama.
Ellinah Wamukoya, 61, sasa atahudumu kama askofu mpya wa kanisa hilo katika ufakme wa Swaziland, moja wapo ya nchi zinazokisiwa kufuata siasaa za kihafidina.