Sura
imeniparama kwa maumivu ya Dora mimi ni mzazi so ilinigusa mnooo! Yatima wanateswa
jamani, lakini watu wanasahau kua yatima na wajane ni jicho la Mungu aliye hai,
fanya ufanyacho malipo ni hapa hapa ulimwenguni.
Dora baada ya kuunguzwa kwa maji moto na vitu vyenye moto hakupelekwa hospitalini, hivyo binamuye akaanza kumtibu kwa madawa ya kienyeji na kusababisha mkono ulio juu kuanza kukakamaa kwa ulemavu!
Mkono wa kulia wa Dora ulikua hauponi bali moto ukawa unazidi kuchimba na kuanza kuoza, nlipokaa karibu naye chozi la uchungu lilinitoka nikipiga picha ukatili huu ungewakuta watoto wangu sijui ningekua katika hali gani.
Huu ni mkono wa kushoto wa Dora ambao kwa sehemu ulikua umekauka kwa tiba hiyo ya kienyeji but hapo kati palikua bado kabisa! majeraha hayo ni cha mtoto twende pamoja ujionee.
Naomba radhi kwa picha hii, lakini uhalisia ni kwamba alichomwa mpaka kwa bibi! kwa kosa gani alilotenda Dora lisilo sameheka? kiasi cha kustahili mateso yote haya? kaka Saumu alikua hamtaki mtoto huyu basi angali mwacha arudi kwa mamaye.
Hili li tumbo la Dora limepona sasa, sijui alichomwa kwa kitu gani kikubwa hivi
Kichwa chake kinaonekana na majeraha ya jalo,la kuchotea moto!
Huu ni mgongo wa mtoto Dora aliye na umri wa miaka 12,katika umri huu Dora ameshaonja mateso kiasi hiki.
Mwili wa Dora una makovu yasiyohesabika, lakini alipigwa mkwara asimwambie mtu juu ya majeraha yake, naye akawa mwaminifu akiteketea kiasi cha kushindwa kufanya baadhi ya mitihani yake kwa majeraha hayo.
Mapaja yake yalivyo
Upande wa Kichwa cha Dora unavyoonekana.
Pembeni hapo ni msamaria mwema aliyemuokoa mtoto Dora almaarufu kama mama mpemba.
MTOTO
DORA ALICHUKULIWA NA BINAMU YAKE KUTOKA MUSOMA NA KUJA KUISHI TEGETA KIBAONI KWA MAKAMBA NA DADAKE BINAMU AITWAYE SAUMU
MASOUD,KWA LENGO LA KUJA KUISHI NAYE BAADA YA BABAKE DORA KUAGA DUNIA.
KWA
HAKIKA DORA AMEISHI KATIKA MATESO MAKUBWA MAISHANI MWAKE, KWANI KAMA MTOTO,
HATAKIWI KUCHEZA NA AKICHELEWA KIDOGO TU ADHABU YAKE NI KUCHOMWA MOTO SEHEMU
MBALI MBALI MWILINI MWAKE IKIWEMO SEHEMU ZA SIRI! UKATILI GANI HUU!
BAADA
YA UKATILI HUO NA KUONA MTOTO AMEANZA KUTOA HARUFU NA HAPONI, SAUMU AKACHUKUA
JUKUMU LA KUTOROKA NYUMBANI KWAKE NA NDIPO TAARIFA ZA MATESO YA DORA ZILIPOVUJA
NA WASAMARIA WEMA AKIWEMO MAMA MPEMBA WA FLAT ZA BOT HAPA DAR-ES-SALAA
ALIPOMCHUKUA NA KUISHI NAYE
SAUMU
MASOUD KASHA KAMATWA NA POLISI WA WAZO
HILL, YEYE NA MUMEWE NA HII NI BAADA YA MUMEWE KUKAMATWA ILI AISAIDIE POLISI, ALIPOULIZWA
WAPI ALIPO MKEWE MUME AKADANGANYA KUA MKEWE KAKIMBILIA MUSOMA, AKAKAMATWA NDIPO
ALIPOFICHUA MKEWE ALIPO
MKEWE ALIPOKUJA WOTE WAKATIWA NDANI MUME ASEME KWANINI
HAKUZUIA UKATILI HUU NDANI YA NYUMBA YAKE! NA MKE ATAJIBU MASHTAKA YAKE YA
UKATILI KWA MTOTO ALO NA UMRI WA MIAKA 12
KWA
SASA MTOTO DORA ANAISHI NA MSAMARIA MWEMA MAENEO YA
MBEZI BEACH SHULE YA MSINGI
MAGOROFA YA BOT.
MTOTO
AMEPELEKWA HOSPITALI NA AMEBANDULIWA MADAWA YOTE YA KIENYEJI, NA AMEPATA
MATIBABU NA MIKONO YAKE ILIANZA KUKUNJIKA
KWA ULEMAVU WA MOTO NA SASA ANAPASWA
KUBEBA VIDUMU VYA LITA TANO, ILI KUINYOOSHA MIKONO.
KESHO
KESI MAHAKAMANI DHIDI YA SAUMU MASOUD KWA UKATILI.
MORE STORY TO COME!
No comments:
Post a Comment