Thursday, July 4, 2013
RAIS WA MISRI APINDULIWA NA JESHI LATANGAZA TAREHE MPYA YA UCHAGUZI
MOHAMMED MORSI aliyekua rais wa Misri
Katika kituo cha televisheni cha AL JAZEERA chumba chao cha habari kimeangazia sakata la huko MISRI ambapo mara baada ya aliyekuwa rais wan chi hiyo MOHAMMED MORSI kupinduliwa na hajulikani alipo mpaka sasa tayari Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo jenerali Abdul Khalil al-Sisi jana usiku alitoa taarifa kupitia televisheni, akitangaza kuwa uchaguzi wa urais utafanyika kabla ya tarehe iliyopangwa, na madaraka ya rais yatatekelezwa na mkuu wa mahakama kuu ya katiba ya nchi hiyo.
Jenerali Sisi alisema mpango uliotolewa na jeshi ni pamoja na mambo manne: uchaguzi wa urais utafanyika kabla ya tarehe iliyopangwa, mkuu wa mahakama kuu ya katiba atashika madaraka ya rais kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo, serikali ya umoja itaundwa, na tume maalumu itaanzishwa ili kujadili marekebisho ya katiba.
Amesema mazungumzo kati ya jeshi la rais Mohammed Morsi yamevunjika, na hotuba iliyotolewa tarehe 2 na rais Morsi haikuweza kutosheleza matakwa ya raia. Bw. Sisi alisisitiza kuwa jeshi la Misri haliwezi kupuuza matakwa ya wananchi wa nchi hiyo, lakini halitaingilia kati mambo ya kisiasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment