Hii
ni picha ya Agness Jerald a.k.a Agness Masogange aliyoiweka kwenye mtandao hv
karibuni akiwa Afrika Kusini.
Wanawake
wawili raia wa Tanzania wametambuliwa kuwa ndiyo wanaodaiwa kuingiza shehena ya
dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 6.8 nchini Afrika
Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza
na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za
Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda
Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald ambaye alisema hajapiga hesabu
ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na
Melisa Edward ambaye alisema
amezaliwa
mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado
wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.
Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini
kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo
wamiliki wa dawa hizo.
Jumapili
iliyopita NIPASHE ilipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya
Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati
zikisafirishwa kutoka Tanzania.
Taarifa
hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki
iliyopita wakitokea Tanzania.
Wanawake
hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na
masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa
hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya
Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.
Baada
ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi.Tukio hilo linatoka
takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu
kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.
Alisema
kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya
dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.
Pia
alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil,
Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha
Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka
kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.
Pinda
alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika
eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.Alisema hivi sasa
mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa
za kulevya.
Alisema
vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa
na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni,
mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.
Maelezo na NIPASHE
No comments:
Post a Comment