MCHUNGAJI wa Kanisa la
Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel
Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.
MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe
akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela
Watoto
wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la
Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba
yao kusomewa kifungo
Mtoto
wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la
Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari
baada ya kesi kumalizika
Waumini
Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika
Watoto
wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la
Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30
Binti anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia
kwa Uchungu baada ya kesi kwisha,sijui ni machozi ya uchungu? ama furaha?
MCHUNGAJI
wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini
Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada
ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema
Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja
katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).
Amesema
Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi
Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131
(1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.
Kutokana
na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta
Mtuhumiwa na
makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga
mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka
limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.
Kwa
upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama
hiyo kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti
na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa
akiwa na Miaka 57.
Pia
alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na
vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo
aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa
kutumia amri ya kutaifisha malishtakiwa.
Hata
hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo
aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake
aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.
Aidha
kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na
viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa
kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa
fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza kuwa Mtuhumiwa
anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika
Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment