Wazazi
waliofika kuwatafuta watoto wao waliokuwa wametoweka.Polisi wa Kenya
wamewakamata zaidi ya wanafunzi elfu moja baada ya kupatikana wakiwa walevi
mjini Nairobi wikendi hii.
Polisi
waliendesha msako katika mabaa na vilabu vya burudani baada ya kupokea
malalamishi kwamba watoto wa shule wamekua wakifurika kuburudika.
Taarifa
zinazohusianaKenyaKwa sasa wanafunzi wengi hawako shuleni baada ya waalimu wa
Kenya kugoma wakitaka serikali kuwalipa marupurupu yao kutokana na ahadi
iliyotolewa kwao na serikali mapema miaka ya themanini.
Mgomo
huo umeingia wiki ya tatu sasa hali iliyofanya wanafunzi kukosa cha kufanya na
hivyo kuanza kwenda kwenye vilabu vya burudani nyakati za usiku.
Katika
kuzima tabia hii polisi mjini Nairobi mwishoni mwa wiki walifanya msako mkali
katika mabaa na sehemu za burudani na kuwanasa watoto zaidi ya 1,000.Polisi
walianza kuwa na wasiwasI wakati visa vya unyang'anyi vilipoongezeka katika mji
mikubwa nchini Kenya.
Wasiwasi
ulizidi wakati walalamikaji walipokuwa wakidai kuwa wanaowapora na kuwapiga
kabari ni kundi la watoto wanaodhaniwa kuwa ni wa shule.Na mabaa na maeneo ya
burudani ilipoanza kufurika polisi wakaona ni wakati muafaka wa kuchukua hatua.
Polisi
sasa wametoa onyo kwa wenye mabaa nchini kenya kuheshimu sheria za biashara.Baada
ya wanafunzi kukosa kurudi nyumbani na wengine kuripotiwa kutoroka katika shule
zao za mabweni wazazi walifurika katika vituo mbali mbali vya polisi kujua
hatma ya watoto wao.
Lakini wengi wa wazazi waliokuwa wamefurika katika kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi walielekeza lawama zao kwa mgomo wa sasa wa walimu unaoendelea
No comments:
Post a Comment