Klabu
ya Liverpool imekubali kwamba inaweza kuumuza mshambuliaji wa kiuruguay Luis
Suarez endapo tu timu inayomtaka italipa kiasi cha paundi millioni 50 - ambayo
ndio thamani ya mshambuliaji huyo kwa mujibu wa Liverpool wenyewe.
Juzi
usiku klabu ya Arsenal ilivunja bank na kuamua kutoa ofa ya £40million kwa
Liverpool kwa ajili ya kumsaini Luis Suarez lakini majogoo wa jiji wakaipiga
chini ofa hiyo na kusisitiza kwamba ikiwa Arsenal wanahitaji saini ya Suarez
basi inabidi walipe fedha ambayo ni thamani ya kweli ya mshambuliaji ambayo
inatajwa kuwa £50m - kwa mujibu wa kocha wa Liverpool Brendan Rogers.
"Ikiwa
Arsenal wanamtaka Suarez, then inabidi walipe fedha ambayo inaendana na thamani
ya kweli ya mchezaji."
Lakini
huku Rogers akisema hivyo imeripotiwa kwamba Arsenal wanataka mshambuliaji
mwenyewe alazimishe kuondoka na kujiunga nao.
Arsenal
wanaamini kwamba Suarez ameshaamua kwa dhati kuondoka Anfield ili ajiunge na
timu inayocheza soka la ligi ya mabingwa wa ulaya.
Na
wanaamini ofa yao ya £40m imefikia fedha ambayo inatakiwa kuvunja mkataba wa
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 - kitu ambacho kinawapa ruhusa ya kuongea
na mchezaji huyo.
Lakini
tatizo kubwa kwa Arsenal ni kwamba wanaamini mshambuliaji huyo angependelea
zaidi kujiunga na Real Madrid ambayo nayo imeomnyesha nia ya kumhitaji.
Real
Madrid jana walimuuza mshambuliaji wao Gonzalo Higuain kwenda Napoli kwa ada ya
uhamisho wa £32 +nyongeza, na hivyo wanaweza kuja kumalizana na Liverpool muda
wowote ikiwa wataachana na mpango wa kumsajili Gareth Bale ambaye anaweza
kuwagharimu kiasi kisichopungua £70m.
No comments:
Post a Comment