Rais
Barack Obama wa Marekani ,leo hii atakamilisha ziara yake ya mataifa
matatu barani Afrika.
Maelfu
ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wamelitokeza katika maeneo mbalimbali na
kusimama pembezoni mwa barabara wakimlaki Rais wa 44 wa Marekani Barak Obama,
ambaye anafanya ziara yake ya kiserikali ya siku mbili hapa nchini.
Miwshoni
mwa juma alikuwako Afrika Kusini ambapo alitowa heshima zake kwa rais wa zamani
wa nchi hiyo Nelson Mandela anayeuguwa.Kiongozi huyo aliyepambana na utawala wa
ubaguzi wa rangi yuko mahtuti hospitalini baada ya kulazwa wiki tatu zilizopita
kutokana na matatizo ya maambukizi ya mapafu. Akihutubia umati katika Chuo
Kikuu cha Cape Town hapo jana Obama alipongeza haiba ya Mandela na kutowa wito
kwa vijana kusonga mbele na hatua za maendeleo barani Afrika.Rais pia
alizinduwa mpango wa dola bilioni saba kuongeza upatikanaji wa huduma za umeme
kwa mataifa sita ya Afrika yakiwemo Tanzania,Kenya,Ethiopia, Liberia na
Nigeria.
No comments:
Post a Comment