MOJA YA NYAKATI AMBAZO HUNGOJEWA KWA HAMU NA
MASHABIKI NI WAKATI AMBAPO DIRISHA LA USAJILI WA WACHEZAJI HUFUNGULIWA . HIKI
NI KIPINDI AMBACHO MASHABIKI HUJAWA NA
MSISIMKO MKUBWA WA KUONA TIMU ZAO ZIKISAJILI MAJEMBE AMBAYO YATAKUJA KUONGEZA
NGUVU KWENYE KIKOSI CHA TIMU HUSIKA .
LEO HII REAL MADRID WANATAJWA KUANDAA DAU LA PAUNDI
MILIONI 85 KWA AJILI YA GARETH BALE LAKINI MADAU HAYA YAMETOKA MBALI TANGU ENZI
AMBAZO BEI YA MCHEZAJI ILIKUWA SAWA NA BEI YA TIKETI KUANGALIA MCHEZO MMOJA .
MCHEZAJI WA KWANZA KUNUNULIWA KWA BEI YA TARAKIMU
TATU ALIKUWA MSCOTLAND WILLIE GROVES AMBAYE ALISAJILIWA TOKA WEST BROWICH
ALBION KWENDA ASTON VILLA KWA PAUNDI MIA MOJA TU .
MIAKA KUMI NA MOJA BAADA YA HAPO ANDY MCOMBIE
ALIVUNJA REKODI YA WILLIE AKISAJILIWA NA NEWCASTLE UNITED TOKA SUNDERLAND KWA
PAUNDI MIA SABA AMBAYO HII LEO HAIFIKII
TIKETI YA MSIMU MZIMA KWENYE UWANJA WA ARSENAL THE EMIRATES.
MMOJA BAADA YA HAPO SUNDERLAND WALITENGENEZA
FEDHA KWA KUWEKA REKODI YA KUMUUZA MCHEZAJI MWINGINE AMBAYE ALIKUWA ALF COMMON AMBAYE KAMA ILIVYOKUWA KWA
ANDY ALIKWENDA KWA MAHASIMU WA JADI WA KLABU HIYO MIDDLESBOROUGH KWA ADA YA UHAMISHO YA PAUNDI ELFU MOJA .
LUIS
SUAREZ ALIKUWA MCHEZAJI WA KWANZA
KATIKA HISTORIA YA MCHEZO HUU KUUZWA KWA ADA AMBAYO ILIKUWA NA TARAKIMU SITA
NDANI YAKE . HAKUWA LUIS SUAREZ HUYU AMBAYE ANATAKA KWENDA ARSENAL KUTOKA
LIVERPOOL BALI ALIKUWA LUIS SUAREZ TOKA BARCELONA AMBAYE ALISAJILIWA NA INTER
MILAN KWA PAUNDI LAKI MOJA NA LEFU HAMSINI NA MBILI , HUO ULIKUWA MWAKA 1961.
MARA YA KWANZA KWA ULIMWENGU WA SOKA KUSIKIA MILIONI
IKITUMIKA KUMSAJILI MCHEZAJI ILIKUWA MWAKA 1975 WAKATI GIUSEPE SALVODI ALIPOTOKA BOLOGNA KWENDA NAPOLI KWA PAUNDI MILIONI
MOJA NA LAKI MBILI , NA HAPA NDIPO MAPINDUZI YA SOKO LA WACHEZAJI YALIPOANZIA .
MIAKA 30 BAADAYE JEAN PIERRE PAPIN ALIKUWA MCHEZAJI WA KWANZA KUSAJILIWA KWA ADA
AMBAYO NAMBARI ZAKE ZILIZIDI KUONGEZEKA . MFARANSA HUYU ALISAJILIWA KWA PAUNDI
MILIONI KUMI TOKA OLYMPIQUE MARSEILE
KWENDA AC MILAN .
HADI LEO REKODI YA USAJILI WA WACHEZAJI KWA FEDHA
NYINGI IMEVUNJWA MARA 41 HUKU KLABU YA REAL
MADRID IKIONGOZA KWA KUVUNJA REKODI YAKE YENYEWE MARA NNE TOFAUTI KWENYE
USAJILI WA LUIS FIGO , ZINEDINE ZIDANE , RICARDO KAKA NA CRISTIANO RONALDO
NA USISHANGAE KUSIKIA GARETH BALE
AKIONGEZEKA KWENYE ORODHA HII.
NCHI YA ITALIA INAONGOZA KWA KUWA NA REKODI NYINGI
ZA KUNUNUA NA KUUZA WACHEZAJI AMBAPO HADI SASA IMESHUHUDIA REKODI 13 ZA MAUZO
NA REKODI 18 ZA MANUNUZI IKIFUATIWA NA ENGLAND AMBAYO IMESHUHUDIA WACHEZAJI
NANE WAKIUZWA TOKA KWENYE KLABU ZA ENGLAND NA KUWEKA REKODI HUKU IKIWA NA
WACHEZAJI SITA WALIONUNULIWA KWA BEI ZILIZOWEKA REKODI NA HISPANIA WANASHIKA NAFASI YA TATU WAKIWA
NA REKODI NNE ZA KUUZA NA REKODI SABA ZA KUNUNUA .
HILO NDIO SOKO LA WACHEZAJI AMBALO LILIANZIA KWA BEI
CHEE YA PAUNDI MIA MOJA AMBAYO NDANI YA SIKU CHACHE ZIJAZO AU PENGINE MIAKA MICHACHE IJAYO
TUNATARAJIA KUIONA IKIONGEZEKA MARADUFU NA KUFIKIA PAUNDI MILIONI MIA MOJA.
No comments:
Post a Comment