Mbalozi
wa Kata 20 wakisubiri kukabidhiwa usafiri wa Baiskeri, nje ya kituo cha shirika
la TARWOC DROP IN.
Naibu
Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki, akikabidhi Baiskeri kwa mabalozi wa
Kata, kutoka Manispaa ya Iringa na Iringa Vijijini.
Baadhi
ya mabalozi wakiwa na Baiskeri zao, baada ya kukabidhiwa rasmi na naibu Meya wa
Manispaa ya Iringa.
Pendo
Luoga (kushoto) Meneja wa kituo cha TARWOC DROP IN- Mkimbizi na Benedict Kibiki
(mwenye suti nyeusi) Ofisa mkuu wa shirika la TARWOC DROP IN- Wakishangilia baada ya
makabidhiano hayo.
MKE
wa waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania mama Tunu Pinda amepongeza
jitihada mbali mbali zinazofanywa na kituo
cha TARWOC DROP-IN cha mkimbizi katika Manispaa ya |Iringa kinachoongozwa mkurugenzi wake mbunge wa
viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mafulu Mng'ong'o kwa kazi nzuri
Mama Pinda alitoa pongezi hizi juzi baada ya
kutembelea kituo hicho na kupokea pongezi nyingi kutoka kwa baadhi ya wanaume ambao
walikuwa wakiongoza kwa unyanyasaji
wa kijinsia kwa wake wao na
wanawake waliokuwa wakinyanyasika
na waume zao ambao kwa sasa wameungana na kuishi kwa amani.
Akitoa
pongezi hizi kituoni hapo mama Pinda
alisema kuwa jitihada zinazofanywa na m
bunge Mng'ong'o katika kutoa elimu ya
ukatili wa kijinsia na kudumisha mausiano kwa wanandoa ni hatua ya kupongezwa na kila mtanzania na
angetamani kuona vituo kama hivyo vinaanzishwa nchi nzima.
Tunu
Pinda alisema kuwa suala la ukatili wa kijinsia
kwa wanawake limeendelea kuchukua
kasi kubwa na kuwa bila jitihada
kama hizo za TARWOC katika kutoa elimu upo uwezekano wa watoto na
wanawake kuendelea kunyanyasika
zaidi.
Hivyo
alisema kuwa ili Tanzania kuendelea
kuwa nchi ya amani ni vema
suala la amani likaanzia katika
familia kwa wanandoa kujenga utamaduni wa kupendana na kuela familia badala ya
kutengana na kusababisha familia kuishi katika mazingira duni.
Hata
hivyo mama Pinda amekubali
kuendelea kuwa karibu na kituo
hicho ili kuwezesha kujulikana zaidi na
kuipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa chini ya mkurugenzi wake Terresa
Mahongo kwa kuendelea kuwa karibu na
kituo hicho bora nchini Tanzania.
Kwa
upande wake meneja wa kituo hicho Pendo
Luoga alisema kuwa toka kituo hicho kimeendelea
kupata mafanikio makubwa katika kuwasaidia watu wanaonyanyasika bila kujali wapi wanatoka .
Huku
afisa mkuu kituo hicho cha TARWOC DROP- IN BenidickKibiki akizsema
kuwa kituo chake kimehudumia zaidi ya
waathirika 1500 wa unyanyasaji na ukatili wa kijisia, na tatizo kuu likiwa ni
uwepo wa mila na destuli potofu, uchumi mdogo pamoja na unywaji wa pombe.
"Tatizo
hili linatokana na baadhi ya mila na destuli zetu zilizopitwa na wakati, hasa
kwa hili la kujiona sisi wanaume kama ndiyo kila kitu, lakini suala la uchumi
nalo linachangia ukatili na unyanyasaji, mtu mwanaume au mwanamke mwenye kipato
duni anafanyiwa unyanyasaji kutokana na hali yake duni, la tatu ni kukosekana
kwa elimu miongoni mwa jamii, kwani baadhi ya wananchi hawana elimu ya namna ya
unyanyasaji," Alisema Kibiki.
Aidha
aliongeza kuwa changamoto inayokikabili kituo hicho cha TARWOC DROP- IN cha
Mkimbizi ni kukosekana kwa ausafiri wa gari, na hivyo kushindwa kuwafikia
wananchi waishio maeneo ya mbali na kituo.
Kibiki
alisema Kata 16 zilizopata baiskeri hizo ni kutoka ndani ya Manispaa ya Iringa
huku Kata 4 za Iringa vvijijini ambazo ni Kata ya Mseke, Ifunda, Kihologota na
Kata ya Kising'a.
Huku
viongozi wa serikali ya mtaaa huo
wakudai kuwa hatua ya kituo hicho kukabidhi usafiri kwa mabalozi ni kusaidia
kupingana na ukatili Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bi Mahongo alisema kuwa jitihada
zinazofanywa na kituo hicho zimeivutia
halmashauri hiyo hivyo
wamelazimika kutoa ardhi zaidi ili kujengwa kituo
kikubwa kitakachowezesha huduma
hiyo kuboreshwa zaidi.
Kwa
upande wake mbunge Mng'ong'o mbali ya
kump;ongeza mama Pinda bado alisem akuwa
lengo lake ni kuhakmikisha mkoa wa Iringa na Tanzania kunakuwepo amani na hakuna mwanake wala mtoto anayenyan yasika.
No comments:
Post a Comment