1.Dirisha la usajili wa
wachezaji barani ulaya limefunguliwa rasmi hapo jana ambapo klabu mbalimbali
ziko huru kufanya usajili wa wachezajiilikuimarisha vikosi vyake . Klabuya
Tottenham Hotspurs tayari imethibitisha kumsajili kiungo aliyeng'aa kwenye
michuano ya kombe la mabara Paulinho ambapo klabu hiyo imeilipa Corinthians
paundi milioni 17 kwa ajili ya kiungo huyo . Kocha wa Spurs Andre Villas Boas
sasa atahamishia nguvu zake kwenye harakati za kusajili mshambuliaji ambapo
Spurs inawatazama Roberto Soldado wa Valencia na David Villa wa Barcelona kama
chaguo la kwanza na la pili huku mshambuliaji Emmanuel Adebayor akiwa njiani
kuihama Spurs ili kuacha nafasi itakayochukuliwa na mmoja kati ya washambuliaji
hao toka Hispania.
2.Wakati hayo yakiendelea
kocha mpya wa Bayern Munich ambaye ameanza kazi hivi karibuni Pep Guardiola
amemruhusu mshambuliaji Mario Gomez kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuweka
wazi kuwa hayuko kwenye mipango yake . Gomez huenda akasajiliwa na klabu ya
Fiorentina ambayo imekuwa ikimuwinda .
3.MICHUANO YA TENIS YA WIMBLEDON IMEENDELEZA HISTORIA YAKE YA
AJABU YA KUSHUHUDIA WACHEZAJI NYOTA WAKITOLEWA MAPEMA BAADA YA HAPO JANA
MCHEZAJI ANAYESHIKA NAFASI YA KWANZA KWA WANAWAKE SERENA WILLIAMS KUTOLEWA NA
SABINE LISKI WA UJERUMANI. WIMBLEDON YA MWAKA HUU TAYARI IMESHUHUDIA MAJINA
MAKUBWA KAMA MARIA SHARAPOVA , CAROLINE WOZNIACKI,ROGER FEDERER NA RAFAEL NADAL
WAKITOLEWA MAPEMA WAKIWAACHA ANDY MURRAY ,DAVID FERRER NA NOVAK DJOKOVIC WAKIWA
NYOTA PEKEE WALIOBAKI KWENYE MICHUANO HIYO .
No comments:
Post a Comment