Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe akihutubia katika
uzinduzi wa mpango wa ufatiliaji ufanisi wa uchukuzi kanda ya kati na nchi
jirani za Burundi, Rwanda, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Uganda, leo
katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam. Mpango huu utakuwa wa miaka minne
na umefadhiliwa na Shirika la Trade Mark East Africa (TMEA).
Wajumbe walioshiriki katika uzinduzi wa mpango wa ufatiliaji ufanisi wa
uchukuzi ambao umejumuisha Mawaziri
wanaoshughulika na Uchukuzi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Uganda,
Rwanda, Burundi na wenyeji Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi wa
Tanzania, Dkt . Harrison Mwakyembe (hayupo pichani). Uzinduzi huo umefanyika
katika hotel ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi Tanzania, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili
kutoka kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango wa ufatiliaji
ufanisi wa uchukuzi katika kanda ya kati na nchi jirani za Burundi, Rwanda, Jamhuri
ya kidemokrasia ya Kongo , Uganda na wenyeji Tanzania. Uzinduzi huo umefanywa katika
hotel ya Serena,jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Waziri wa wa Nchi Uchukuzi
kutoka nchini Uganda, Bw. Steven
Chemoiko Chebroto, na wa pili kutoka
kulia ni Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mitambo wa Burundi, Mhandisi Deogratius
Rurimunzu. Wa kwanza kushoto ni Bw. Scott Allen kutoka Trade Mark East Africa (TMEA)Nairobi.
Waziri wa ya Uchukuzi wa Tanzania, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza
kushoto), Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mitambo wa Burundi, Mhandisi Deogratius
Rurimunzu (mwenye tai nyekundu) na Waziri wa Nchi Uchukuzi wa Uganda, Bw.
Steven Chemoiko Chebroto, wakiweka sahihi kwenye vitabu kuashiria uzinduzi wa mpango
maalum ufatiliaji ufanisi wa uchukuzi katika ukanda wa kati
na nchi jirani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, akiweka sahihi
katika kitabu cha mpango muhimu wa ufatiliaji ufanisi wa uchukuzi katika kanda
ya kati na nchi jirani za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo na Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo(kulia), akibadilishana
mawazo na Muwakilishi Mkazi wa Trade Mark East Africa Tanzania, Bi Tonia
Kandiero, wakati wa uzinduzi wa mpango ufatiliaji ufanisi wa uchukuzi katika kanda ya kati
na nchi jirani za Rwanda, Burundi,Uganda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
No comments:
Post a Comment