Dora
akiwa na nuru mpya ya matumaini, mara baada ya kubambuliwa majikisamvu yalikua
yamebandikwa katika majeraha ya moto, kwa sasa anaendelea na matibabu na
ameanza kurejea furahani na michezo yake inaendelea kama kawaida.
Mwanzoni
Dora alikua hatabasamu hata kidogo kwa maumivu, lakini baada ya matibabu ndipo
tabasamu liliporejea katika uso wake, nuru inanonekana na hata urembo wake ulidhihirika dhahiri.
MONIKA SAHILE ni Mama mdogo
wa mtoto huyo ambaye anaishi mkoani Tanga na amekuja Dar es Salaam baada ya
kupata taarifa za kuunguzwa kwa mtoto huyo.
Dada Zubeida mwenye mtandio wa njano akiwa na mamake mdogo, yeye ni dada wa Dora ambaye naye ana masahibu yake tele! ntakupa hapahapa
Mtu na dadake bwana! hapana chezeiya kabisa
Mi hupenda sana watoto! basi Dora nadhani alinigundua! akaanza kunifanyia vituko vya hapa na pale, bwana wangu! mtoto alinipa swagga mwenyewe nlistarehe!
Nami sikua na haraka nilimpa nafasi ya kutosha, akajiachia alivyoweza na kamera yangu! kamera hiyo haikufanya ajizi.
Mikono
hii ilikua haiinuki kabla ya matibabu stahiki kupatikana!
Mtoto alijigeuza alivyotaka kuonesha furaha yake
Hapo je. ujue ni yeye mwenyewe anaelekeza, nkampa raha bana wee
swaggar baby
mtu na dadake bwana, na matumaini tele
Bi Kauthar, msamaria mwema alomuokoa mtoto huyo mpaka hatua aloifikia leo.
No comments:
Post a Comment