Wednesday, July 3, 2013

VIWANJANI







1.barani ulaya taarifa za usajili wa wachezaji zimezidi kumake headlines ambapo tetesi nyingi zimekuwa zikizungumzwa .
kwa mujibu wa mtandao wa espn klabu ya manchester uited ina imani kubwa a kukamilisha usajili wa nahodha wa timu ya taifa ya vijana ya hispania thiago alcantarra ambaye vyanzo kadhaa ndani ya united vimesema kuwa atasajiliwa hivi karibuni .
taarifa zaidi zinasema kuwa united imefikia makubaliano ya kimsingi na mchezaji huyo na kilichobaki ni kukamilisha masuala madogo .

2.wakati hayo yakiendelea klabu ya bayern munich  hapo jana iliwatambulisha rasmi wachezaji wawili iliowasajili mbele ya waandishi wa habari .
bayern iliwatambulisha mario gotze aliyesajiliwa toka borusia dortmund na beki jan kirchoff toka mainz zikiwa zimepita siku kadhaa tangu kocha mpya pep usrdiola kuanza kazi ya kuifundisha bayern .
utambulisho huo hata hivyo uliwaudhi wadhamini wa bayern munich ambao ni kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya adidas baada ya wachezaji waliotambulishwa kuonekana wamevaa fulana zenye nembo ya mpinzani wa adidas kwenye biashara ambaye ni kampuni ya nike .

No comments:

Post a Comment