Idadi
kubwa ya vijana wanaojiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya inaweza
kupungua ama kuisha kabisa endapo waathirika wa utumiaji wa dawa hizo
watatumika kutoa elimu kwa vijana wenzao ambao bado hawajaingia katika janga
hilo ambalo ni hatari sana kwa nguvu kazi ya taifa.
Tone
Media kupitia TANGA YETU imefika katika kituo cha watumiaji wa dawa za kulevya
(Rehab, SOBER HOUSE) jijini Tanga ambao wanatoa mbinu na elimu ya kutorudia
kutumia dawa hizo ambazo zinaathiri na kugharimu maisha ya vijana wengi.
Ibrahimu
Daga ambaye ni Mwenyekiti wa Rehab SOBER HOUSE jijini Tanga anasema kituo hicho
hulea watu 35 na kuwapatia elimu ya namna ya kuishi bila kurudia matumiazi ya
dawa hizo, mafunzo ambayo hudumu kwa miezi minne.
Anasema
kuwa kituo hicho hakijapata msaada wowote kutoka serikalini hasa mamlaka
zinazohusika na dawa za kulevya na kwamba kinajiendesha kwa michango ya wazazi
wa waathirika.
“Tunahitaji
sana kuungwa mkono na serikali hasa katika upande wa kupata chakula kwa hawa
vijana tulionao, lakini katika mipango ya muda mrefu tunahitaji eneo kubwa
kwajili ya kujenga Rehab itakayochukua watu wengi zaidi” anaeleza Ibrahim
Meneja
wa Rehab hiyo Salum Amour anasema mahitaji makubwa katika rehab hiyo ni kupata
elimu ya ujasiliamali, biashara, kilimo na ufugaji kwa waathirika hao ili baada
ya kumaliza muda wa Rehab wawe na uwezo wa kuendesha maisha yao hata baada ya
kurejea katika hali zao za kawaida.
Miongoni
mwa shughuli wanazojifunza ni usafi na kupika.
Vijana hawa wanatoa ujumbe mzito kwa vijana
wenzao, wakisema USIJARIBU KUFIKIRIA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA NI HATARI.
Meneja
wa Rehab hiyo Salum Amour (mwenye t-sheirt nyekundu) akizungumza na mwandishi
wa habari
Nyumba
inayotumika kuhifadhia vijana hao
Viongozi
wa serikali kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Kitaifa ni jukumu lenu sasa
kuhakikisha kuwa mnaunga mkono jitihada za Rehab hii kwa kusaidia kuboresha
hudumu ikiwemo chakula ili malengo ya kumaliza tatizo la mateja mitaani
yafanikiwe, PESA ZA DAWA ZA KULEVYA NA UKWIMWI ZINAKWENDA WAPI??? Walengwa ndio
hawa hamuwaoni?
No comments:
Post a Comment