wahenga wa kizungu wana msemo usemao
hivi . be careful of what you wish for , maana yake ni kwamba unapaswa kuwa
makini kwa kile unachotamani kukipata , wakati mwingine kinaweza kisiwe na
manufaa unayofikiri au kutarajia , klabu ya real madrid imezoeleka kama klabu
ya kifalme ambayo moja ya sera zake kwa miaka yake yote imekuwa kusajili
wachezaji nyota wenye hadhi ya kuchezea klabu hiyo , wakati rais wa sasa
florentino perez alipoingia madarakani aliendeleza sera hii kwa muundo mpya wa
galacticoz . sera hii imeshuhuda nyota kama luis figo , zinedine zidane ,
ronaldo de lima , ricardo kaka na hata cristiano ronaldo . kama mipango
ingeenda vyema huenda jina la neymar lingeongezeka kwenye orodha hii , lakini
pamoja na kutoa ofa kubwa kuliko wapinzani fc barcelona neymar mwenye
alipendezwa kuchezea barca na akaitolea nje los merengues .
kutolewa nje na neymar kulimfanya rais
florentino perez kujawa na hasira na kuhamishia dhamira yake kwa jina moja la
mchezaji aliyeiwasha moto vilivyo ligi kuu ya england msimu uliopita , huyu si
mwingine bali ni gareth frank bale .
bale ambaye alianza maisha yake ya
soka kama beki wa kushoto amekuwa akibadilshwa nafasi mara kadhaa , kwa muda
alikuwa amezoeleka kama winga lakini msimu uliopita alichezeshwa nyuma ya
mshambuliaji , yalikuwa maamuzi ya kiunfundi ambayo yaliinufaisha tottenham na
kuboresha kiwango cha mchezaji mwenyewe maradufu hali iliyovifanya vilabu kama
real madrid kumtolea macho .
tukirudi kwenye uhalisia wa maisha
ndani ya real madrid swali la kujiuliza ni moja , ni nani anataka kumsajili
bale , je ni kocha mtaliano carlo ancelotti au ni rais florentino perez ambaye
mara zote amekuwa mstari wa mbele kusajili nyota walioko moyoni mwake .
mahitaji ya kifundi na mahitaji ya kibiashara kwenye timu moja ni vitu viwili tofauti , kocha carlo ancelotti amezungumza kuwa
anataka kumchezesha mchezaji nyota wa real madrid cristiano ronaldo kwenye
nafasi ambayo atakuwa karibu na lango la timu pinzani tofauti na nafasi ya kushambulia toka pembeni
ili awe na madhara zaidi , ni nafasi hii hii ambayo gareth bale aling’aa akiwa
na totenham msimu uliopita .
tayari msimu huu madrid imesajili
nyota kama isco ambaye kama ronaldo na
bale hushambulia akitokea pembezoni mwa uwanja
na bado timu hii ina mshambuliaji ambaye anatarajiwa kupambana kupata
nafsi kwneye kikosi cha kwanza ambaye ni karim benzema huku kukiwa na viungo
washambuliaji kama mesut ozil na wengineo , usajili wa bale hakika utaleta
changamoto kubwa ya nafasi kama sio mvuragano ambao badala ya kunufaisha madrid
huenda ukaharibu mambo ,
suala la biashara ya jezi
limezungumzwa kama moja ya sababu za perez kuhangaika sana kupata sahihi ya
gareth bale ili auze jezi kutokana na umaarufu wake .
tayari real imetoa ofa ya paundi
milioni 85 kwa ajili ya gareth bale ambaye moyoni mwake ameridhia kujiunga na
klabu hiyo kizingiti pekee cha kumzuia asijiunge ni mfanyabiashara mwenye
historia ya usugu kwenye mazungumzo ambaye ni mwenyekiti daniel levy .
ujio wa bale ambao tuna angalau asilimia 75 ya uhakika wa
kutokea kwake utakuwa mbaraka kwa real
madrid au utakuwa laana ya galactico ambayo itaendelea kutafuna mipango ya
kibiashara inayoingiliana na mipango ya kiufundi , tusubiri kupata jibu la
swali hili
No comments:
Post a Comment