Andy
Murray amekuwa Muingereza wa kwanza kushinda taji la Wimbledon tangu mwaka
1936, ikiwa ni zaidi ya miaka 77.Murray amemfunga Novak Djokovic raia wa Serbia
kwa seti tatu kwa kwa bila katika mchezo wa fainal za wanaume za michuano ya
tenesi ya Wimbledon.
Murray
amemshinda mchezaji anayeorodheshwa wa kwanza duniani Novak Djokovic kwa seti tatu
kwa bila za 6-4, 7-5, 6-4.Andy Murray amesema anashindwa kuamini kile
alichokifanya kwani mechi hiyo ilikuwa ngumu, huku joto likiwa kubwa lakini
anashukuru ameweza kumaliza mechi hiyo kwa ushindi muhimu kwake na kwa taifa.
Hili
ni taji la pili la michuano mikubwa ya tenesi duniani maarufu kama Grand Slam
baada ya kushinda lile la Michuano ya wazi ya Marekani.Muingereza wa mwisho
kushinda taji la Wimbeldon ambalo hufanyika mjini London kila mwaka alikuwa ni
Fred Perry aliyeshinda taji hilo kwenye michuano ya mwaka 1936.
Mwaka
jana Andy Murray alipoteza mchezo wa fainali ya michuano ya Wimbledon kwa
kufungwa na Roger Federer.Malkia wa Uingereza, Elizabeth wa pili amemtumia
ujumbe wa Pongezi Andy Murray kwa ushindi wake katika mechi ambayo ilishudiwa
pia na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon.
No comments:
Post a Comment