Wednesday, July 10, 2013

SHORT CUT ITATUUA WAJAMENI!



hatariii kiwira wilayani rungwe watumia mikokoteni kusafirishia nyama iliyotoka machinjioni. huu ni mkokoteni unaotumika kusafirisha nyama ya mifugo mbalimbali iliyochinjwa machinjioni na kupelekwa kwenye mabucha ya kuuzia nyama kiwira wilayani rungwe.

 


hii ndiyo hali halisi na mikokoteni hii ndiyo inayotumika kubeba mizigo mbalimbali ya wateja ikiwemo mbolea kwa ajili ya matumizi ya mashambani
 Kwa raha zao nyama inaingizwa buchani tayari kwa mauzo! na wanawake wengine tuna tabia ya kupika nyama bila ya kuichemsha, katika mazingira haya kuna usalama kweli?
Kwa kawaida yapo magari maalum ya kubebea nyama, sasa sijui yako machache huko Kiwira? au ni nini?unafuu katika usafiri? du!
Bila taarifa kua nyama hiyo ilibebwa katika mazingira yaso stahili! wateja wamejazana buchani kununua nyama hiyo na kwenda katika matumizi ya vitoweleo.
Kama kawa kama dawa.


No comments:

Post a Comment