Mwenyekiti
wa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro ambaye pia ndiye
Mkuu wa Mkoa Mbeya akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza mkuu
wa mkoa Mbeya akiongea na waandishi wa habari
Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya hatimaye yatoa ufafanuzi na kupigilia
Msumari maamuzi ya Kamati ya Ushauri (RCC) ya kupeleka Makao makuu ya Mkoa mpya
Mkwajuni Wilayani Chunya.
Akitoa
maamuzi ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa
Mbeya, Abbasi Kandoro ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa Mbeya akiongea na vyombo
vya habari ofisini kwake amesema Kamati imeridhika na ushauri uliotolewa na Kamati ya
Ushauri iliyofanyika Julai 4, Mwaka huu.
Kandoro
amesema lengo la kukutana na kamati ya ulinzi na usalama ni kutokana na kuibuka
kwa maneno toka kwa baadhi ya Wananchi ambao wanadai maamuzi yaliyotolewa na Kamati
ya kupeleka Makao makuu ya Mkoa Mpya Mkwajuni Wilayani Chunya hayakuzingatia
vigezo vya umbali wa baadhi ya maeneo.
Amesema
katika kuliletea ufafanuzi jambo hilo Mkuu huyo wa Mkoa alidai kuwa baadhi ya
wajumbe wa kamati ya Ushauri wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri na Wenyeviti
wao wameitwa ili kutoa maelezo kwenye kamati ya Ulinzi kama endapo mapendekezo
yaliyotolewa na RCC hayakuzingatia matakwa ya wananchi.
Ameongeza
kuwa baada ya Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa kuridhika na maelezo ya wajumbe
hao imebariki na kuamua kuwa mapendekezo ya Kamati ya Ushauri yabaki vile vile
kwa Mkoa mpya kuwa Songwe inayotokana na Mto Songwe uliopita kila Wilaya
zinazounda Mkoa huo ambazo ni Momba, Mbozi, Chunya na Ileje.
No comments:
Post a Comment