VIONGOZI WA NIGERIA NA
CHINA MJINI BEIJING
China
imekubali kutoa mkopo wa dola bilioni 1.1 kwa Nigeria ili kufadhili ukarabati
wa miundo msingi.Mkataba huu umeafaikiwa wakati wa ziara ya Rais Goodluck
Jonathan mjini Beijing,ambapo alikutana na mwenyeji wake Xi Jinping.
Fedha
hizi zitasaidia ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege na kujenga miji minne na
njia mpya ya reli.China inawekeza kwa kiwango kikubwa Barani Afrika ambapo pia
imekua ikipata raslimali za mafuta na madini.
Nigeria
inaongoza kwa kuzalisha mafuta Afrika lakini kwa miaka imekua na miundo msingi
mibovu, huku mamilioni ya raia wake wakiishi kwa umasikini. Bw. Xi amesema nchi
mbili zinashirikiana kwa minajili ya kuboresha maisha ya watu wake.
Rais
Jonathan anaongoza ujumbe wa wawekezaji wa Nigeria huko China na ziara ya siku
nne itasaidia kuleta mshikamano wa karibu wa kibiashara.
Kampuni
za ujenzi za Ki-China zimeanza kujenga barabara nchini Nigeria, kwa kandarasi
ya dola bilioni 1.7.China kwa upande wake inatarajia kupata mapipa laki mbili
ya matufa ghafi kutoka Nigeria ifikapo mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment