Maafisa
wa polisi wa Kenya wakikagua shehena ya pembe za ndovu zilizokamatwa kwenye
bandari ya Mombasa siku ya Jumatatu (tarehe 8 Julai). Pembe hizo zilinaswa
kwenye kontena moja lenye urefu wa futi 20 lililokuwa likisubiri kusafirishwa
kwenda
Maafisa
wa forodha wa Kenya siku ya Jumanne (tarehe 9 Julai) walitoa taarifa za kina za
shehena haramu ya pembe za ndovu iliyokamatwa kwenye bandari ya Mombasa,
inayokisiwa kuwa tani 3.2, moja ya shehena kubwa kabisa katika historia ya siku
za karibuni.
Odinga
aomba msaada wa kimataifa kupambana na majangiliPolisi wa Kenya wamsaka
mtuhumiwa kuhusiana na mlipuko wa NairobiNairobi kuweka kamera za uchunguzi
ifikapo mwezi JanuariMaafisa wa Kenya wanasa tani 2 za pembe za ndovu kwenye
bandari ya Mombasa "Pembe hizo
zina uzito wa kilo 3,287.2 zikiwemo nzima 382 na vipande 62," alisema
msemaji wa Huduma ya Wanyamapori Kenya (KWS) mjini Mombasa, Paul Mbugua, kwa
mujibu wa Capital FM ya Kenya.
Mbugua
alisema hakuweza kukisia thamani ya mzigo huo kwa sababu hakuna bei maalum ya
pembe za ndovu kwenye soko la magendo.
Pembe
nyengine zilikuwa na uzito wa takribani kilo 60, zikiwa zimetokana na wale
wanaoitwa "tembo wakubwa", alisema afisa wa forodha Fatuma Yussuf,
kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Shehena
nyengine ya tani 1.5 ya pembe za ndovu, ambayo pia ilikuwa isafirishwe kwenda
Malaysia, ilinaswa mjini Mombasa wiki iliyopita, na kuchochea onyo kutoka kwa
Shirika la Kimataifa la Biashara ya Viumbe Walio Hatarini (CITES). Nchi sita za
Afrika pia zilipokea onyo kutoka CITES kuongeza hali ya hadhari dhidi ya
magendo kwenye bandari zake.
No comments:
Post a Comment