Wednesday, July 24, 2013
KWA TAARIFA YAKO TU!
kama ulikua unadhani hapa Dar Dala dala zinapark hovyo! mh cheki hizi matatuu nchini Kenya zilivyokaa, japo wao wame advance unapata net kwenye matatuu, ili kuvutia wateja, hapa bongo mpoooo? tutafika lini huko? na tumo kwenye karne ya teknolojia,sayansi na utandawazi?
Matatuu za kenya zime pimpiwa kinoma, kuna muziki munene ndani yake na kama hiyo haitoshi kuna dvd screen ukiwa safarini uienjoy!
Pamoja na hayo kua matatuu zinavutia na huduma zingine za ziada! abiria wawapo safarini huwa roho juu kwani madereva huendesha kwa speed mno! na nauli hazitabiriki hubadilika badilika kila leo.Ndipo sa waziri wa usafiri wa wakati huo 2004 Joh Michuki akaamure matatuu ziwe na mikanda ya vitini na pia matatuu ziwekewe vidhibiti mwendo
Badala ya kua na wafanyakazi zaidi ya kumi wa matatuu moja1 sasa wanapaswa kua wawili tu! nadhani daladala za bongo kuna cha kujifunza kutoka kwa matatuu za Kenya, mnatujaza kama ng'ombe, wenzetu kule no kusimama wala kushika bomba! abiria ni 25 au 15 tu na mkanda unajifunga, sheria tele! hapa?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment