Tuesday, July 23, 2013

WAFANYAKAZI WA TTCL MBEYA WATAKIWA KUSHIRIKIANA.

Hilo limesemwa na Mfanyakazi wa Shirika hilo, Mrs. Hellen Maringo wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake watumishi wa TTCL Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya Kumwaga baada ya kupata uhamisho na kuhamia Jijini Dar Es Salaam.

Mwenyekiti wa umoja huo  Kaundime Mfinanga akitoa neno  kusisitiza umoja.

Muda wa kumpa zawadi muagwa.

 Furaha iliyoje kwa utumishi uliotukuka

Pongezi mpendwa maana unastahili

Maakuli na masangweji

Wafanyakazi wa Shirika la Simu (TTCL), Mkoa wa Mbeya wameaswa kuendeleza ushirikiano uliopo miongoni mwa Watumishi ili kuleta ufanisi wa Kazi na shirika kwa ujumla.

Hilo limesemwa na Mfanyakazi wa Shirika hilo, Mrs. Hellen Maringo wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake watumishi wa TTCL Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya Kumwaga baada ya kupata uhamisho na kuhamia Jijini Dar Es Salaam.

Maringo amesema kuondoka kwake kusiwe mwisho wa umoja wao hivyo wanapaswa kuyaendeleza mazuri yote waliyokuwa wakishirikiana  awali na kuongeza kuwa mipango ya Munguni mingi ipo siku atarudishwa tena Mbeya hivyo ni mategemeo yake kwamba akirudi atakuta bado umoja unaendelea.

Hafla ya kumwaga Mfanyakazi huyo ilifanyika  katika Hoteli ya Beaco iliyopo Forest Jijini Mbeya ikiongozwa na Mwenyekiti Kaundime Mfinanga, na Katibu wake Stellah Mndanga wakisindi

No comments:

Post a Comment