Monday, July 8, 2013

KWA MPANGO HUU! TUTAKWISHA KABLA YA WAKATI!




Dk.Andrey Votyakov muhusika wa tukio hilo.


 RUSSIA

Tukio hili lilitokea huko Urusi (Federal Cardo-Surgery Centre) baada ya daktari pichani kumshambulia mgonjwa wa moyo kwa kumpiga ngumi kadhaa upande wa kushoto ambapo moyo upo bila kujua kuna kamera iliokua ikimrekodi.Baada ya muda mfupi mgonjwa huyo alifariki.

Baada ya kuhojiwa daktari huyo alisema alipatwa na hasira sababu wakati walipokua wakiingia  kumuhudumia, mgonjwa huyo alianza kumuita majina mabaya na pia alimpiga ngumi. Baada ya hapo mgonjwa huyo alifungwa mikono kitandani na aliendelea kutoa maneno mabaya dhidi ya madaktari.

Uchovu aliokua nao daktari huyo baada ya kufanya kazi kwa masaa 24 ulimsababisha kushindwa kuzuia hasira yake na kuanza kumshambulia mgonjwa kwa ngumi upande moyo ulipo.Hakujua kama kuna kamera iliyokua ikimrekodi.

Polisi waliiona video ya tukio hili kupitia mtandoa wa intaneti na kuanza kufuatilia hatimaye kugundua ukweli wa tukio hili. Hata hivyo datkari huyu alikiri kosa na kulaumu uchovu aliokua nao na kuwaomba radhi familia ya marehemu. Familia bado haija zungumza chochote juu ya tukio hili.

Mahakama ya nchi hiyo inatarajia kumpa hukumu daktari huyo hivi karibuni pamoja na faini. Tukio hili lilitokea mwezi Februari 2013 lakini liliwekwa wazi hivi karibuni.
Ifuatayo ni video ikionesha jinsi Daktari alivyokua akimpiga mgonjwa huyo.

No comments:

Post a Comment