Friday, July 12, 2013

TAARIFA YA JWTZ KUHUSU SIKU YA MASHUJAA MWAKA HUU



JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

 

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linaadhimisha siku ya mashujaa kila tarehe 25 Julai, ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka mashujaa waliopigana na kushinda vita ya Kagera mwaka 1978/1979.

Maadhimisho hayo  hufanyika mara moja kwa mwaka, na mwaka huu yatafanyika tarehe 25 Julai 2013 katika mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba kwenye makaburi ya mashujaa yaliyopo Kaboya.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Sambamba na mgeni rasmi, watakuwepo viongozi waandamizi wa Serikali, vyombo vya 

Ulinzi na Usalama, vyama vya siasa, taasisi za dini na taasisi mbalimbali za kiraia.Vyombo vya habari vinaalikwa kushiriki katika maadhimisho hayo ambayo ni muhimu kwa Taifa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764742161

No comments:

Post a Comment