Hapa ni mbezi kanisani kwa Yusuphu, majira ya saa kumi na moja kasoro ndipo nnlipokutana na Wiseman Mwaluvanda Mwakyusa,alikua nyapinyapi'
Hoi magoti yameviiimba
Viatu vimekwisha visiginoni, miguu ilikua inawaka moto.akisimama alikua anayumba mbaya
Swagger hakuna, no tabasamu yaani ukimsimamamisha anaona unamchelewesha.
Pamoja na kukatishwa tamaa kwa maneno na ujumbe mfupi, safari iliendelea MBEYA TO DAR
Hapa na pale alikua akipewa mkono na hata chochote kwa safari
watu wali show love kwa kupiga naye picha hapa na pale njiani
Wasamaria wema walikua wanampa walau kitu kidogo kwa mahitaji ya njiani, hapo ni Mbezi Louis
Nyuma alicha gumzo yeye, huyooo anaendelea na safari mdogomdogo
Jimmy Francis wa Pb team ambaye ni producer akiwa ameshikilia mic ya clouds tv alipokua akihojiwa Wiseman mbele ya daraja la mtombezi
Ilibidi tumsindikize Wiseman kituo cha afya BOCHI MEDICAL CENTER kwa Msuguri ili apate huduma ya kwanza na huyu ni Dk Matemu akimpa huduma ya kwanza na mapumziko mafupi, asante sana Bosch
Juma Katunda wa Clouds Tv akichukua matukio hatua kwa hatua
Sehemu zote za kiungo kutoka nyayoni hadi mapajani vilivimba
Maumivu yalikua makali mno! lakini ilibidi
Huu ndo muonekano wa hospitali ya Bochi Medical Center, nilifurahishwa sana na utayari na huduma yao, kiasi cha kumsaidia Wiseman arejee barabrani
JUMA KATUNDA NA Juma pilot wetu wakiliangalia jengo safi la hospitali
Hapa ni baada ya huduma ya kwanza, na kuruhusiwa kuendelea na safari, basi akavaa viatu vyake
Juma akaona kiwingu kilizidi akaomba ya peke yake hiyo bababaaa!
Safari ikaendelea, hapa ni kituo cha korogwe-kimara
Picha zilikua zinagombewa mno! basi wakati napiga picha nika sheck.
No comments:
Post a Comment