Thursday, May 31, 2012

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Matumizi ya Tumbaku





Licha ya Shirika la Afya Duniani WHO kutoa ripoti inayobainisha kuwa tumbaku inaua takribani watu milioni 6 kila mwaka na ni moja ya vyanzo vya maradhi na vifo vinavyoweza kuzuilika duniani!
Makampuni ya tumbaku yanatumia hela na mbinu chafu kudhoofisha vita dhidi ya matumizi ya tumbaku limesema shirika la afya duniani WHO.
Mbinu hizo ni pamoja na kuchagiza mlolongo wa hatua za kisheria dhidi ya serikali ambazo zimekuwa msitari wa mbele kwenye vita dhidi ya bidhaa za tumbaku, kuongeza chumvi kuhusu umuhimu wa kiuchumi wa bidhaa za tumbaku na kutotilia maanani thibitisho la kisayansi la madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya tumbaku.
Ikiwa ni katika maandalizi ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku ambayo huadhimishwa Mai 31, WHO imezitaka serikali kuwa makini kutokana na ongezeko la mashambulizi ya makampuni ya tumbaku Dr Douglas Bettcher ni mkurugenzi wa idara ya WHO ya mradi wa kuachana na tumbaku.
WHO inasema tumbaku inauwa takribani watu milioni 6 kila mwaka na ni moja ya vyanzo vya maradhi na vifo vinavyoweza kuzuilika duniani


Charles Taylor asukumwa jela miaka 50



Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor amehukumiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita miaka 50 jela .. Mwezi uliopita Charles Taylor alipatikana na makosa ya kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2002.Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80. Ingawa Charles Taylor amesisitiza hana hatia yeyote na anatarajiwa kukata rufaa. Mwandishi wa BBC aliyeko The Hague Anna Holligan anasema rufaa dhidi ya hukumu hii huenda ikachukua miezi sita. Akitoa hukumu hiyo Jaji Richard Lussick amesema dhuluma zilizotekelezwa nchini Siera Leone zilikuwa za kinyama zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu. Mahakama maalum ya Kimataifa inayochunguza dhuluma za kivita nchini Sierra Leone ilimkuta Taylor na hatia ya makosa 11 dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.Taylor amekuwa Rais wa kwanza kuhukumiwa kwa makosa ya vita na Mahakama ya Kimataifa tangu kesi za Nuremurgs dhidi ya watawala wa Kinazi baada ya Vita Kuu vya Pili duniani. Charles Taylor amelalamikia upande wa mashtaka kwa kuwatisha mashahidi katika kesi dhidi yake. Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kwa kuwapa silaha waasi na kubadilishana na almasi. Kesi dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Liberia inasikilizwa The Hague kwa hofu kwamba kufanyika kwake Sierra Leone huenda kukazua vurugu katika kanda hiyo. Taylor anatarajiwa kuhudimia kifungo chake nchini Uingereza.

Wednesday, May 30, 2012

Kaite Middleton anavyo Shine kwa mama


KATE MIDDLETON.

Duchess huyu mumewe anatamani mama yake aamke akutane na mrembo huyo, lakini kutokana na ukweli kua aliyekwenda harudi, anayazuia machozi yake na kuupa ukweli uhalisia! ki ukweli hata mimi nampenda sana dada huyu na mumewe.



                                      naipenda sana hii couple jamani! naamini ndo maana William            anatamani mama yake angekuwepo anaone mke alonaye!


kizuri kupita yote ni tabasamu la huyu dada! adamu na unyofu awapo kati kati ya watu, ana nipa raha sana!



sooo niice hajivuni kuingia katika familia bora, naamini ukiwa karibu naye utakua na fahari sana!



                       mwepesi kua karibu yako na hata kukugusa! wow she's so sweet!



                                               hisia zake hazifichiki



huleta tabasamu kwa yeyote aliye karibu yake! baba mkwe ameguswa! akaachia tabasamu, Carmilla vipi mama?




                                               wow ame win hatimaye




Queen si rahisi kuzoeleka,ukapiga naye story lakini kwa mrembo huyo hapindui bibi huyo mwenye kuadhimisha  Diamond Jubilee yake




Dimpoz zake zinafaa kwa poz! hahahh




meno yake yaliyosafishwa humpa uthubutu wa kusogea karibu na wageni mashuhuri na kuteta nao bila kusahau tabasamu lisilo kauka usoni mwake, na kiukweli ana smile vizuri sana! 
 jifunze ili usizeeke haraka ndo siri ya tabasamu.



unyofu wake miye hoi, amefundishwa na akafundishika, twasubiri mtoto tu kwa sasa.mh lol hahah 



Tuesday, May 29, 2012

Happy Birthday My brother


Alex Kussaga , leo ni birthday yake kiukweli Alex ni mtu wa peke yake! kwa jinsi anavyo ishi na watu mjengo! unafki kwake mwiko, happy birth day mybrother from another mother! hahahah Let the God decorate each ,golden ray of the sun reaching u,with wishes of success,happiness and prosperity 4 u,wish you a super duper happy birthday brother


wapili kwa leo ni


ni Marco Chali producer wa muziki wa kizazi kipya kwa lable ya Mj Records! nimesha fanya naye kazi hi's cool, na anaijua kazi yake . happy birthday bro!

Mahaba Yalovunda!



Zilipendwa


hebu itazame hiyo picha hapo juu! wawili hao ni wazazi wana watoto lakini lakuvunda halina ubani, bi mkubwa amempata dereva ajuaye gari yake yenda mbio, ukimtazama bwan'kaka kama amechoka flani na bado ana hitaji penzi la bibi huyo! JL!!!ukiitazama hiyo picha kwa umakini mkubwa utaona jinsi body language kwa upande wa Marc Anthony inavyojidhihirisha kua ana mhitaji hata leo! bi mkubwa akapotezea maji juu ya paji la uso wa Marc so hakufanikiwa kugusanisha midomo na wa Marc! ila mkono aliushika kama zamani!



baba ako sasa pale kati duu macho hayabanduki kwa mtalaka wake! mamaa full kupotezea! lakini kuonesha kuenzi  lililokua penzi lao na ndoa kwa ujumla wake ! Marc Anthony bado ana pete ya ndoa katika kidole cha pete! na waweza kuiona katika  kidole cha pete, hao wameanzisha! wapo wengi wanaowapotezea wapenzi wao! hebu twende pamoja ushuhudie pale mpenzio anapokupotezea, take care! usijufumbishe macho kuonesha hisia kwa mwenzio kuna hasara yake! oh fumba kisungura shauri yako! utachekwa! hahahah twendeeeeeeeee




mama ako sasa! waone  Nicole Scherzinger  na Lewis Hamilton , Nicole kafa kaoza kwa Lewis ! muone alivyojilaza katika bega la mshkaji kama kinda! na jamaa ana uhakika wa penzi la bi mkubwa huyo cheki alivyo mkumbatia! aka hataki hivi! hahahah na hii kwangu mimi si dalili nzuri! bi mkubwa kajiachia we unajifanya kama huhusiki vile?!



Ben Affleck naye alikua akimpotezea hivyo hivyo Jenifer Lopez ni kama alikua akituma ujumbe kwa mtu aliye pembeni yao hivi! inaumaje?, Jl  akamwepuka! isiwe taabu babu eh nenda kwa hao hao alah!



kiboko ya wanaume wadaku wanaowapotezea wapenzi wao ni Paris Hilton, alipoona hapewi attantion na jamaa yake Benji Madden akaamua kumtopisha na kumpa mtazamo kua nipo hapa shingo feni ya nini? hata mimi ni mwanamke kama wao na zaidi ya yote tumekuja pamoja tulia! hahahhh uh mboni mambo?



Shantelle Houghton yeye aliamua kuchukua mkono wa mshkaji Prestone  na kumuelekeza shika hapa! lakini hiyo haikufaa kitu na haibadili hisia na mtazamo wake kwako kama uonavyo sura inaongea yenyewe! mh



Noah Lebenzon amshindwa kuficha kua mapenzi hayapo tena kati yao! cheki demu amejipanga kupokea mijibusu lakini mshkaji ana msanifu  Ana Ortiz, aiseee!

kiukweli mapenzi matamu,lakini machungu kama shubiri, kila mmoja huonja kwa wakati wake! wakati ukifika hutaacha kuona rangi !













Gaitanaaaa from Africa!!!



be my guest! iangalie kiutuvu!

Ubaguzi wa rangi katika sanaa Ulaya



Kama ulidhani ubaguzi wa rangi umekwisha! basi utakua umejisahaulisha kidogo tu! kwa maifa machache na watu wachache wenye ubinafsi uliopindukia wanauendeleza ubaguzi wa rangi. kuna shindano la kisanii linaloelekea kwenye kilele nalo linalenga kusherehekea usanii wa kitsch (barani Uropa),  shindano hilo  la muimbaji bora la Eurovision kila linapofanyika huzua hisia za kichochezi ambazo sio kawaida kutokea kwingineko.
Na hivyo ndivyo ilivyo mwaka huu wakati shindano hilo likielekea kileleni. Hisia za ubaguzi wa rangi tayari zimeanza kuzungumziwa kabla ya shindano hilo kufikia fainali.
Chama chenye msimamo mkali cha Freedom Party, nchini Ukrain, kilimshambulia kwa maneno msanii Gaitana - ambaye ni mzaliwa wa Congo na ambaye anawakilisha Ukraia kwenye shindano hilo.







"Mamilioni ya watu watakaokuwa wanatizama fainali ya shindano hilo, watajionea Ukraian ikiwakilishwa na mtu ambaye sio wa rangi yetu" ndivyo alivyosema Yuri Syrotyuk, ambaye chama chake kianajiandaa kwa uchaguzi wa wabunge baadaye mwaka huu."Ukrain itaonekana kama nchi iliyo katika eneo la vijijini huko barani Afrika" aliongeza kusema Yuri Syrotyuk,
Hata hivyo baadaye alikana madai ya ubaguzi wa rangi, akisema kuwa alikuwa anakosoa tu kutokuwepo uwazi katika namna mwakilishi kutoka nchini humo alivyochaguliwa.
Lakini matamshi yake yalikemewa sana nchini Ukraine na vyama vyote rasmi vya kisiasa na wasanii wengine mfano Vitaly, Volodymyr Klitschko na mshindi wa shindano hilo mwaka 2004, Ruslana.



Gaitana, atamenyana na wenzake katika awamu ya nusu fainali Alhamisi usiku, na amesema kuwa matamashi hayo ya ubaguzi wa rangi yameonyesha tatizo hilo lilivyokithiri nchini Ukraine.
"Nimekerwa sana na matamshi hayo, kwa sababu Ukrain ni nchi yenye demokrasia ambako watu wenye unyenykevu na utu wanaishi" alisema Gaitana.
Babake Gaitana ambaye ni raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, alisomea katika mji mkuu wa Ukrain, Kiev, ambako alikutana na mamake Gaitana na kumuoa.
Muda mfupi baada ya kuzaliwa kwa Gaitana, mwaka 1979, familia yake ilihamia Congo-Brazzaville ambako waliishi kwa miaka mitano. Hata hivyo wazazi wake walitalakiana lakini mamake Gaitana alirejea naye nchini Ukrain.




Gaitana huandika nyimbo zake mwenyewe na anajioana kama mchanganyiko wa tamamduni mbili kwa sababu marafiki zake nchini Congo wanasema mziki wake una mizizi ya Kiafrika.
Fainali ya shindano hilo itafanyika nchini Azerbaijan na kutazamwa na watu milioni 125 kote barani Uropa. Wengi wanaona kama Gaitana ana nafasi nzuri ya kushinda shindano hilo.Atamenyana na washindani kutoka nchini Sweden, Uturuki, Romania, Italia na Ugiriki.
ALL THE BEST GAITANA






30 waachiliwa kwa dhamana Zanzibar









Viongozi wawili wa kundi la Uamsho waliokuwa wanashikiliwa na polisi wa Zanzibar kwa zaidi ya siku mbili pamoja na baadhi ya wafuasi wao wameachiliwa kwa dhamana katika mahakama ya Mwanakwerekwe huko Zanzibar.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo ya kisiasa, kuachiliwa kwa viongozi hao ambao walikuwa wanakabiliwa na kosa la kuandamana bila kibali kunaweza kukomesha uhasama wa takriban siku mbili baina ya wafuasi wa kundi hilo na polisi.
Taarifa zinaeleza kua hali ilianza kuwa shwari  Zanzibar baada ya kuachiliwa kwa dhamana kwa wafuasi takriban thalathini wa kundi la Uamsho waliokuwa wanashikiliwa na polisi mjini humo kwa tuhuma za kuandamana bila kibali.
Miongoni mwa waliopata dhamana hiyo ni Sheikh Mbaruku Saidi Khalfan na Musa Juma Musa wote wakiwa viongozi wa kundi hilo ambao kukamatwa kwao kumeleta kizazaa huko Zanzibar.
Mbele ya Hakimu wa mahakama ya Mwanakwerekwe majira ya saa nne asubuhi Jumatatu, baada ya kusomewa mashtaka ya kufanya mkusanyiko haramu katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, watuhumiwa hao kwa pamoja walikana tuhuma hizo.Baadaye wakili wa watuhumiwa hao aliwaombea dhamana, ombi ambalo lilikubaliwa bila pingamizi lolote.
Kukamatwa kwa viongozi hawa kumeleta sokomoto kubwa mjini Unguja hasa baada ya wafuasi wa kundi hilo kuamua kuandamana kwa lengo la kuishinikiza polisi kuwaachilia.Hali iliyosababisha vuta nikuvute baina ya wafuasi hao na polisi ambao wamekuwa wakitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.
Uamsho ni kundi la kidini ambalo limejipa jukumu la kuwaelimisha wazanzibari kuhusu suala la muungano hasa wanapotoa maoni yao katika Tume ambayo inakusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Hata hivyo, taarifa zisizothibitishwa zinasema, kundi hilo limejikita zaidi katika kuwahamasisha wananchi kuupinga muungano.

RIRI Asherehekea Miaka 7 ya Pon de Reply



 Happy Aniversary Pon de Reply

                 



Habari  wadau wa blog hii!e bana eh! Kama umeweka mazoea ya kusherehekea miaka kadhaa ya kuzaliwa kwako basi leo nakushawishi walu uwe unasherehekea vitu ulivyonavyo maishani kwa kuweka kumbukumbu za vitu hivyo na ukifika wakati wa kusherehekea basi ufanye hivyo!
Nimeamua kukushawishi kwani mwanamuziki nguli wa miondoko ya pop duniani Rihanna ameamua kusherehekea miaka 7 ya single yake ya Pon de pLay  ambayo aliipakua mnamo mwezi kama huu mwaka wenye kumbukumbu katika taifa hili wa 2005 wakati huo RIRI akiwa na miaka 17 tu na akaifanyia promo album  yake ya kwanza iitwayo “Music Of The Sun”.
 Na hii ni kauli yake aliyoitupia kwenye account yake ya twitter  RIRI name namnukuu kwa lugha ya biashara na mawasiliano  duniani“Happy birthday Pon de Replay! Today marks 7years #eliteNaviS**t I love y’all foreverrrrrrrr (sic),”.

Single hiyo ya ‘Pon De Replay’  imekamata #2 katika chati za majuu nazungumzia kwa mama haha sijui kijana wa leo kama unaufahamu msemo huo, sisi wa zamani tunajua ni wapi , ila kwa kifupi kwa mama ni  UK  na kama hiyo haitoshi single hiyo imebamba katika chati za marekani maarufu kama Hot 100 tangu ilipoanzishwa .

Katika miaka yake yote saba katika tasnia ya burudani Rihanna amekwisha kupakua album 6 na kufanikiwa kuuza rikodi zake milioni 25 duniani kote.kwa upande wa singles RiRi ameshauza kopi milioni 60 na ameshaachilia zingine 40 na amesha fanya ziara ya kuizunguka dunia mara 4.
Mmoja wa jirani zake RIRI anajisikia fahari kuona maendeleo ya jirani yake yakipanda siku hadi siku, na wakadi single hiyo ya Pon de Reply ikitoka jirani yake huyo alikua na miaka 7 tu,na sasa jirani huyo ana miaka 17 umri ambao alikua nao RIRI alipokua na achilia single hiyo,na anasikia fahari kwa mafanikio ya jirani yake huyo,kizuri zaidi kutoka kua jirani yake hadi kua muimbaji wa kimataifa,muigizaji,mwanamitindo ambaye amekwisha uza mamilioni ya kazi zake duniani na kufanikiwa kupata nafasi ya kazi zake 12 kushika namba 1,kupata tuzo 5 za Grammy awards, tuzo 18 za BMA’S, na idadi inaongezeka,ingawa jirani huyu hajataka kuachia jina lake lakini ametoa pongezi hizi! Happy 7 Years Rihanna!

Monday, May 28, 2012

Serena Asusia Mapenzi


                                                           Serena williams

Mchezaji Tennesi mashuhuri duniani,Serena Williams, amesusa kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi kwa miaka 10 ijayo.

Serena Williams mwenye umri wa miaka (30) amefikia uamuzi huo baada ya uhusiano na mpenzi wake rapa Common,kujaa karaha zilizomfanya achukie suala zima la mapenzi.
na namnukuu Nimeacha kua na uhusiano,uhusiano umenifanya niumie sana na kukata tamaa.nimeamua kujiondoa kwenye mapenzi kwa miaka 10 ijayo! je ataweza? nafsi inatamani ,mwili unataka lakini ubongo wake utakua umeelekezwa kutotamani.
uamuzi huo unakuja baada ya dada huyo kudai kua amekua na bahati mbaya katika mapenzi,na anaseam kama unajitahidi na mambo hayaendi vizuri, unaachana na suala hilo mara moja, na kwa kufanya hivyo anaamini atakua na muda mzuri zaidi na tennesi,anapenda kua uwanjani, na hicho ndicho anachoishi kukifanya.



                                                     walipokua mapenzini

Ajioa Kukwepa Upweke





bwana na bibi ndo yeye



Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ametoa kali ya mwaka kwa kuamua kuandaa harusi na kujioa yeye mwenyewe kanisani.
Nadine Schweigert mwenye umri wa miaka 36 amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari nchini Marekani baada ya kuandaa harusi na kujioa yeye mwenyewe ambapo yeye ndiye alikuwa bi harusi na yeye pia ndiye aliyekuwa bwana harusi.Nadine ambaye ni mkazi wa Fargo, North Dakota nchini Marekani alijioa mwenyewe kwenye sherehe iliyohudhuriwa na jumla ya watu 40.
Alikula viapo vya ndoa mbele ya umati huo wa watu ambapo mwisho wa viapo alipuliza busu angani badala ya hali iliyozoeleka ya bibi na bwana harusi kubusiana.Harusi hiyo ilifuatiliwa na fungate la nguvu (honeymoon) kwenye hoteli moja mjini New Orleans.
Akiielezea ndoa yake hiyo kwenye kipindi cha televisheni moja nchini humo, Nadine alisema kuwa hivi sasa anajihisi ni mwenye furaha sana na ndoa yake imeweza kuyabadilisha maisha yake toka kwenye huzuni na kuwa mwenye furaha sana.
Nadine alisema kuwa aliamua kujioa mwenyewe baada ya ndoa yake na mumewe aliyezaa naye watoto wawili ilipovunjika na watoto wake kuamua kwenda kuishi na baba yao.
Nadine alisema kuwa alipita kipindi kigumu sana cha machungu ya kuvunjika kwa ndoa yake lakini baadae aliamua kukaa chini na kutafakari maisha yake badala ya kujiingiza kwenye ulevi ili kupoteza mawazo.
Nadine aliongeza kuwa ndipo alipogundua kuwa furaha ya kweli na mtu anayempenda sana ni yeye mwenyewe hivyo akaamua kujioa yeye mwenyewe na hivi sasa haitaji tena mwanaume kwenye maisha yake.Nadine aliongeza kuwa katika maisha yake haya mapya amekuwa akijitoa out mara kwa mara na amekuwa akijinunulia zawadi yeye mwenyewe.

Mark Webber aibuka mshindi Monaco


Dereva kutoka Australia Webber aliweza kuongoza mashindano ya Monte Carlo kuanzia mwanzo mwisho
Mark Webber aliibuka mshindi katika mashindano ya langalanga ya Monaco GP siku ya Jumapili, huu ukiwa ushindi wake wa pili katika kipindi chini ya miaka mitatu, na akiwatangulia madereva Nico Rosberg kutoka Ujerumani, na wa timu ya Mercedes, na Fernando Alonso kutoka Uhispania, na wa timu ya Ferrari.
Dereva kutoka Australia Webber aliweza kuongoza mashindano ya Monte Carlo kuanzia mwanzo hadi mwisho ,Webber ni dereva wa Red Bull.
Dereva wa McLaren, Lewis Hamilton wa Uingereza, kuna wakati aliweza kujikita katika nafasi ya tatu, lakini akapitwa na dereva wa Ferrari Alonso, na vile vile Sebastian Vettel wa Red Bull, ambao walitumia mbinu bora za kuhakikisha walidumisha kasi yao na kumpita.
Wakati mmoja Alonso maksudi alibaki nyuma, ili kuokoa magurudumu yake, na ili yaweza kunasa barabara vyema katika dakika za mwishomwisho alipohitaji kasi kabla ya kuvifikia vituo vya kupata huduma ya gari kurekebishwa.
Mbinu hiyo hatimaye ilimsaidia kufanya vyema, kwani Webber na Hamilton waliposimama katika raundi ya 29, raundi mbili zaidi ya Rosberg, Alonso aliweza kwenda mzunguko mmoja zaidi, na akienda kwa kasi sana wakati huo.Mbinu hiyo ilimwezesha kumtangulia Hamilton.
Dereva mwingine wa Uingereza, na wa timu ya McLaren, Jenson Button, alipata mashindano hayo kuwa magumu, na baada ya muda mfupi alilazimika kuondoka mapema.
Ushindi wa Mark Webber umeandikisha historia mpya katika mashindano ya Formula 1, kwa kuwa ni mara ya kwanza madereva sita tofauti kuibuka washindi baada ya mashindano sita ya msimu.
"Ninahisi nimefanikiwa kufanya maajabu," alielezea Webber kutoka Australia.”"Ni siku ya ajabu kwa timu na mimi binafsi, na nimefurahi sana kupata tena ushindi hapa.”
Kufuatia matokeo hayo, Alonso wa timu ya Ferrari sasa anaongoza katika kuwania ubingwa wa dunia, akimtangulia Vettel na Webber kwa pointi tatu.
Hamilton anateremka kutoka nafasi ya tatu hadi nne, akiachwa nyuma na Alonso kwa pointi 13

Rwanda yashutumiwa kuchochea uasi DRC


waasi DRC
Umoja wa Mataifa umesema uasi ulioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo unachochewa na nchi jirani ya Rwanda.Taarifa ya ndani ya umoja huo ambayo BBC imeiona, inaishutumu Rwanda kwa kuwapatia silaha na askari waasi wa Congo.
Taarifa hiyo imezingatia mahojiano na waasi ambao wanasema waliandikishwa Rwanda kwa kisingizio cha kujiunga na jeshi la nchi hiyo, lakini walipewa silaha na mafunzo na kuvuka mpaka kwenda kupigana Congo.
Taarifa hiyo inasema mmoja wa waasi ni wa cheo cha chini.Uasi huo, ambao ni wa hivi karibuni katika eneo hilo lenye mgogoro, ulianza mwezi Aprili baada ya baadhi ya maafisa wa jeshi la Congo kuasi

Argentina yakumbwa








Kimbunga chenye ukubwa wa kipimo wa  6.3, kimekumba kaskazini  mwa Argentina


katikati ya kaskazini ya Argentina

Lady Gaga avunja Onesho lake Baada ya Kupokea Vitisho


Lady akiongoza makamuzi kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards



Mwanadada mbunifu wa maonesho ya jukwaani Lady Gaga ameahirisha tour yake ya kimuziki Asia baada ya kutakiwa kufanya hivyo na watu wa usalama wa Indoneshia baada ya tishio kutoka kwa viongozi wakuu wa kiislamu nchini humo.
Nyota huyo wa miondoko ya pop alikua akiipigia promo  album yake ya born this way ball ,ilimpasa kuahirisha show yake baada ya kuelezwa ukweli kua akitia mguu wake katika jiji la Jarkata basi ajue watashughulika naye.
Chama cha kutetea uislam The Islamic Defenders Front (FPI) kilitoa msimamo wao juu ya mavazi ya Lady Gaga kua yana shawishi ngono na uchezaji wake vinaweza  kuwatia majaribuni vijana wa Indoneshia na waislamu walio wengi katika taifa lao.na wakatamka wazi kua Gaga akijitia kichwa ngumu basi watamdhuru na wakamwita wakala wa shetani ambae huvalia sidiria tupu na chu** tu.
Pamoja na matangazo kibao kufanywa lakini management ya Gaga  wanatazama kitisho hicho kwa jicho la tatu na kuita kua ni lengo la kushusha moto wa tamasha la june 3 atakalofanya Gaga , ndipo mwanasheriaMinola Sebayang  ambaye ni promoter wa Big Daddy Promotion alipomtaka Gaga kuahirisha tour hiyo na kusema kua hawatawasamehe walowatisha .
Chama hicho cha FPI kimeendelea kueleza kua Indoneshia italindwa na kuepushwa na dhambi zitakazo sababishwa na shetani huyo,japokua chama hicho chenye mrengo wa kiislam kutoa vitisho hivyo! Raia wa nchi hiyo tiketi zipatazo 50,000 zilisha uzwa na ilitegemewa kua ndo tour kubwa kuliko zote kuwahi kufanywa Asia.
Management ya Gaga imeshangazwa na wana usalama wa Indoneshia walipowataarifu kua kutokana na sababu za kiusalama Tour ya Gaga katika nchi yao haitowezekana,serikali ya nchi hiyo ilishaonesha ushirikiano ,lakini tishio hilo ni kubwa kuliko mtu kukosa kibali cha kuingia katika nchi hiyo.
Saa chache kabla ya tangazo hilo kutolewa,mwanamuziki Lady Gagag mwenye follower milioni 25 katika account yake ya twitter alitupia kauli hii "There is nothing Holy about hatred."
Mwenyekiti wa chama hicho cha FPI ambaye anadai ana followers milioni 7 kwenye akaunti yake ya twitter wamefurashishwa na uamuzi wa Lady Gaga kutokwenda nchini kwao, awali FPI  wamesha shambulia  clubs na pubs kibao  na wamewataka mashabiki wa Lady kuacha kulalama na wajirekebishe na kama haitoshi waache kumwabudu shetwan.
FPI wanaendelea kufunguka kuwa wao kama wao walisha nunua tiketi kama 150 hivi ili kupata nafasi ya kua sehemu ya washiriki ili wapate nafasi nzuri zaidi ya kusimamisha show hiyo endapo ingelazimu kufanywa.
Kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali na pia mwenye dhamana ya mahusiano ya kidini  waziri Suryadharma Ali amefurahiwa na vuguvugu hilo la kumsimamisha Gaga kwa kufanikiwa kufanya hivyo na akasherehekea kufanikiwa huko na kusema kuahirishwa kwa tour hiyo ni kwa manufaa ya nchi yao  na kueleza kua Indoneshia burudani haikataliwi mradi iwe ya kistaarabu  na si vinginevyo  no!
Pamoja na FPI kumtia mkwara Lady Gaga, kuna waliotangulia kufanya show nchini humo kama Beyonce na Pussycat Dolls wao walisoma alama za nyakati na kuvaa vyema ili tu wapaafom na walifanikiwa.
Pamoja na hayo yote Maelfu ya followers wa Gaga walimtumia tweet kibao wakimtaka Gaga asihofu chochote bali aendelee na mipango yake kama kawaida, kijana mwenye umri wa miaka 17 Agus Murdadi amesubiri kwa  miezi kadhaa kumuona Lady Gaga ,na akaeleza hisia zake kua ameshtushwa sana na taarifa kua Lady Gaga hata kwenda tena nchini mwao kwa mtazamo wake Lady ni mbunifu na sio mhamasishaji ngono.na kuahidi kumtumia tweet Lady kua asihofu aende tu nchini mwao na kusema polisi wanaweza kuwazui FPI wasifanye chotechote nay eye kwa nafsi yake anawachukia FPI.
Lady Gagag ana show zipatazo kama 3 hivi , huko Singapore wiki hii  kabla hajakwea pipa kuelekea New Zealand na Australia na baadae Ulaya kumalizia tour yake.


                                                           Lady Gaga

Mtumishi wa Papa Benedict akamatwa


Basillika hiyo.



kwenye duara ni mtuhumiwa Paolo Gabriele akiwa na Bosi wake Papa Benedict wa xvi



Jana ilikua ni siku ya kumuabudu Mungu kwetu sisi wakristu, wengi walijitokeza katika nyumba za ibada, kwa wakatoliki kama mimi mkuu wetu ni Papa Benedict wa xvi, makao yake makuu yako Roma nchini Italia.kuna jambo huko mjengoni ambapo ,Polisi wa Vatikani wamemshtaki rasmi mtumishi wa Papa Benedict, katika kesi inayohusu wizi wa nyaraka za siri.
Paolo Gabriele - ambaye alikua akitumika kwenye fleti ya papa - amezuwiliwa Vatikani, na ameruhusiwa kuonana na mawakili wawili.
Wakuu wanachunguza vipi, katika miezi ya karibuni, magazeti ya Utaliana yalipata nyaraka ambazo zinaeleza mashindano kati ya wakuu wa kanisa - kisa ambacho kimeanza kuitwa 'Vatileaks'.
Inaarifiwa kuwa Papa Benedict ameshangazwa na kusikitishwa kuwa mtumishi wake mmoja amekamatwa.




Mkuu wa Benki ya Vatikani alitolewa kazini Alhamisi, kutokana na kashfa hiyo.

Friday, May 25, 2012

Picha za Siku ya Leo


Mungu kweli anaumba! kindege kinatabasamu hadi kimefumba macho, halafu Mungu akampamba kwa hiyo rangi juu ya macho yake sijui niseme nyusi? kazurije? wow asante Mungu kwa uumbaji.



wako katika mazoezi ya yoga, Mungu ni waajabu sana wanyama wakifundishwa kwa Lugha zetu wanaelewa na kufuata maelekezo yote uwapayo.mbwa ni rafiki muaminifu na mlinzi mzuri sana mi huwa napenda aina ya mbwa kama wale wa feed Force.






Picha ya Leo


hii ni picha ya leo nimependa alivyopambwa! zaidi sana kicheko chake ndege huyu!

Will Smith Asafishwa


Willy Smith

juzi kazi willy Smith alibusiwa na tv Presenter na yeye Willy akamtumbuiza kwa kofi! naamini unakumbuka au siyo? so  jamaa ameomba radhi na kuahidi kutorudia kumbusu na badala ya akikutana naye atamsalimia kwa mkono tu




Will Smith akifafanua namna tukio lilivyotokea na alikua akihojiwa na Mr Letterman



 na hapo chini jamaa naye anafunguka juu ya tukio hilo.


JOHN MNYIKA AIBUKA KIDEDEA MAHAKAMA KUU JANA



Mbunge wa jimbo la Ubungo CHADEMA Mh. John Mnyika akiwa amebebewa na wanachama wa chama hicho mara baada ya mahakama Kuu ya Tanzania  kumtangaza mshindi katika  kesi ya uchaguzi iliyokuwa ikimkabili  kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Ubungo iliyofunguliwa na mpinzani wake Hawa Ng'humbi wa chama cha CCM.


John Mnyika akionyesha ishara ya ushindi akiwa na wapambe wake pepembeni wakielekea Ubungo kwa ajili ya mkutano wa hadhara



John Mnyika akiutubia wafuasi wa chama chake katika jimbo lake la Ubungo mara baada ya kuwasili



Jeshi la polisi likihakikisha ulinzi unaimarika katika mahakama hiyo leo.

Thursday, May 24, 2012

Tuzo Za BET zaja








Host ndo huyo naamini mwamfahamu kupitia thamthilia ya  Isidingo The Need Samuel L. Jackson


Tuzo za BET zaja na zitakua mwezi July 1, jijini Los Angeles nchini Marekani.wafuatao watachuana kuwania tuzo kama mtiririko huo hapo chini unavyo ainisha.

Best Female R&B Artist:
Marsha Ambrosius
Beyoncé
Mary J. Blige
Melanie Fiona
Rihanna
Best Male R&B Artist:Chris Brown
Bruno Mars
Miguel
Trey Songz
Usher
Best Group:Bad Meets Evil
Diddy-Dirty Money
Maybach Music Group
Mindless Behavior
The Throne (Jay-Z & Kanye West)
Best Male Hip-Hop Artist:Big Sean
Drake
J. Cole
Lil Wayne
Rick Ross
Young Jeezy
Best Female Hip-Hop Artist:
Diamond
Nicki Minaj
Brianna Perry
Trina
Best International Act: UK:
Estelle
Labrinth
Emeli Sandé
Sway
Wretch 32
Best New Artist:A$AP Rocky
Big Sean
Diggy
Future
Meek Mill
Video of the Year:Beyoncé - 'Countdown'
Beyoncé - 'Love On Top'
The Throne (Jay-Z & Kanye West) - 'N***as in Paris'
The Throne (Jay-Z & Kanye West) featuring Otis Redding - 'Otis'?- Usher - 'Climax'
Viewers' Choice Award:
Beyoncé - 'Love on Top'
Chris Brown - 'Turn Up the Music'
Drake featuring Lil Wayne & Tyga - 'The Motto'
Mindless Behavior -  'Hello'
The Throne (Jay-Z & Kanye West) featuring Otis Redding - 'Otis'
Wale featuring Miguel - 'Lotus Flower Bomb'
Best International Act: Africa
Camp Mulla (Kenya)
Ice Prince (Nigeria)
Lira (South Africa)
Mokobe (Mali)
Sarkodie (Ghana)
Wizkid (Nigeria)
Best Collaboration:
Beyoncé featuring J. Cole - 'Party'
Big Sean featuring Kanye West & Roscoe Dash - 'Marvin & Chardonnay'
DJ Khaled featuring Drake - Rick Ross & Lil Wayne - 'I'm On One'
Drake featuring Lil Wayne & Tyga - 'The Motto'
The Throne (Jay-Z & Kanye West) featuring Otis Redding - 'Otis'
Wale featuring Miguel - 'Lotus Flower Bomb'



Beyonce

bibi huyo hapo juu ameingia katika category 6 tofauti tofauti



Kanye West

yeye amekua nomineted mara 7



Chris Brown

anawania tuzo tatu ikiwemo ya Best Male RnB Artist  na ataburudisha katika sherehe hiyo ya utolewaji wa tuzo za BET


mabibi hapo juu wenye vibweka karibu sawa wanawania tuzo moja category tofauti



                                  Big Sean maetwaa tuzo 2 ikiwemo ya Best New Artist

tusubiri kuona  watazikwaa hizo nomination?