Ilichukua
dakika 28 Manchester United kupata goli kupitia mchezaji wake machachari Robin
Van Persie a.k.a RVP akiifunga timu yake ya zamani Arsenal The Gunners goli
moja lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Ingawa Arsenal alicheza vizuri sana
lakini hawakufanikiwa kupata goli na mechi ya hiyo ni mechi ya pili kwa timu ya
Asernal kupoteza toka msimu wa ligi hiyo ulipoanza.
Manchester United imefikisha
pointi 21 ikiwa nafasi ya 5, lakini Arsenal imeendelea kushikilia usukani kwa
kuwa na pointi 25 ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 23 na Southampton yenye
pointi 22, Chelsea anapointi 21.
No comments:
Post a Comment