Friday, November 22, 2013

P-SQUARE WATUA BONGO TAYARI KWA ONESHO LEADERS CLUB KESHO




Mwanamuziki wa kundi la P - Square, Paul Okoye akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarake Nyerere, Tayari kwa ajili ya kutoa burudani kwa Watanzania, Msanii huyo aliambatana na Pacha wake Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P- Square. Wasanii hao wameambatana na wenzao 13 ambao watatoa burudani jumamosi ya tarehe 23 Novemba. Tamasha hilo limeandaliwa na East African Radio na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 
Wakiwa wametua na wanatoka nje ya uwanja wa ndege wa JK

Mwanamuzikiwa kundi la P- Square Peter Okoye akizungumza na waandishi wa habari,
mapema baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka katika bendi yao.  Pamoja nao katika picha ni pacha wa msanii  huyo Paul Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P - Square .

MenejaUhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akizungumza na wasanii Peter na Paul Okoye punde baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini Nigeria.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu  na Afisa Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo  Ibrahim Kaude, wakiongozana na wasanii Peterna Paul Okoye punde baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini Nigeria.
 

Via: gabrielkilamlya.blogspot.com

No comments:

Post a Comment