Ndugu wanahabari.
BAADA ya kumshukuru na kumtukuza mwenyezi Mungu mwingi wa
rehema. Natanguliza salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu mwanazuoni na
mwanaharakati mwenzangu Dkt Sengondo Mvungi aliyetangulia mbele ya Haki siku
chache zilizopita huko Afrika ya kusini.
Ndugu zangu wanahabari.
Wengi mnanifahamu na kuifahamu vema historia yangu katika
utendaji kazi na utumishi wa umma wa Watanzania. Nimekuwa nikiitumikia nchi
yangu kwa kipindi kirefu katika Nyanja na sekta mbali mbali kuanzia Darasani
mpaka kwenye siasa.
Kwa msingi huo, mimi Profesa Juma Kapuya, siku zote
ninajikuta mwenye wajibu endelevu wa kuendelea kulitumikia Taifa langu kila
siku mpaka kufikia mwisho wa Nguvu zangu.
Ndugu wanahabari.
Hivi karibuni nikiwa huku jimboni kuendelea na shuhuli za utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kumezuka Tuhuma kadhaa zilizoelekezwa dhidi yamgu zikiasisiwa na wanasiasa wenzangu wa ndani na nje ya chama changu ili kudhoofisha juhudi na utendaji wangu wa kila siku.
Hivi karibuni nikiwa huku jimboni kuendelea na shuhuli za utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kumezuka Tuhuma kadhaa zilizoelekezwa dhidi yamgu zikiasisiwa na wanasiasa wenzangu wa ndani na nje ya chama changu ili kudhoofisha juhudi na utendaji wangu wa kila siku.
Tuhuma hizo zisizokuwa na kichwa wala miguu na pia
kutokuwa na ukweli wowote, wamekuwa wakizitoa kwa kumtumia msichana anayedai
amefanyiwa vitendo visivyofaa na mimi. Mimi simfahamu na sijui hizi shutuma
zinatokea wapi.
Ndugu wanahabari,
Kwa tamko hili ninapenda kuwaambia kuwa nimefedheheshwa
sana na uwezo mdogo wa kisiasa unaofanywa na hawa watu kwa kuwa dhamira yao
haitatimia.
Napenda niwakumbushe ndugu zangu kwamba tunaelekea kwenye
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na wapinzani wangu wameanza kunichafua ili
nionekane sifai.
Ninapenda kuwaambia watanzania na wananchi wa jimbo langu
kuwa wanatakiwa wazipuuze taarifa hizi kwa kuwa hazina ukweli wowote na kwamba
ni za kutungwa zenye lengo la kunidharirisha na kuniondolea heshima yangu
niliyojijengea kwenye jamii kwa kipindi kirefu sasa. Waswahili wanasema dawa ya
mjinga ni kumpuuza.
Na hili linajidhihirisha zaidi kwa habari hii kuandikwa
na chombo kimoja tu cha habari kinachotumiwa na chama kimoja cha siasa na
baadhi ya wanasiasa wa chama changu wasiokitakia heri chama chetu, naomba kuwashukuru
na kuwapongeza vyombo vingine vya habari kwa umakini wenu wa kuwa na nauelewa
wa kutoandika kitu bila kukifanyia uchunguzi na kubaini ukweli ulivyo.
Chombo hiki cha habari kiliwahi kuripoti mwaka jana kuwa
kuna mitambo imeingizwa nchini inayoweza kuandika ujumbe na kisha kuufanya
uonekane umetoka kwenye namba Fulani, kwa kipindi kile sikuwaelewa, lakini sasa
ninawaelewa na nimewaona kuwa wako sahihi na wao ndio waliouingiza mtambo huu
na sasa wameamua kuutumia dhidi yangu kwa kutengeneza meseji na kuzihusianisha
na mimi.
Ninaamini ukweli utawaumbua muda si mrefu.
Ndugu wanahabari.
Nimeijenga heshima yangu na familia yangu kwa jamii yangu kwa kipindi kirefu mno, kwa hivyo siwezi kuruhusu heshima niliyoijenga kwa miongo kadhaa karibiwa na kupotezwa na watu wachache tena kwa muda mfupi namna hii.
Nimeijenga heshima yangu na familia yangu kwa jamii yangu kwa kipindi kirefu mno, kwa hivyo siwezi kuruhusu heshima niliyoijenga kwa miongo kadhaa karibiwa na kupotezwa na watu wachache tena kwa muda mfupi namna hii.
Hivyo basi nimechukua hatua za kisheria kuhakikisha
heshima yangu inaendelea kulindwa na utu wangu unaheshimiwa.
Nimemwagiza mwanasheria wangu afungue kesi na tayari
amewashitaki watu wote wanaohusika kwenye mpango huu na tayari wameshapokea
taarifa ya kuitwa mahakamani.
Nitaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote
watakaoendelea kutaka kujipatia umaarufu ama wa kisiasa au wowote ule kwa
kutumia jina langu.
Hayo yote ni kwa kuzingatia ukweli kwamba nchi yetu
inaendeshwa kwa misingi ya kisheria na kufuata na kuheshimu haki na wajibu
wakila mmoja wetu.
Kwenye hilo ninawaambia ‘’janja yao nimeigundua, na
hawatafanikiwa’’.
Ninatoa Rai kwa yeyote mwenye kuona hilo jambo lina
ukweli alipeleke kwenye vyombo husika ili lishuhulikiwe kwa mujibu wa sheria na
sio kutumia vyombo vya habari kuchafuana.
Mwisho ninasisitiza kuwa nitaendelea kuilinda na kuitetea
heshima yangu niliyojijengea kwa jamii kwa muda mrefu sasa na sitaruhusukuiona
ikiharibiwa na wajanja wachache kwa maslahi yao binafsi.
Tuendelee kuijenga nchi yetu,
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Tanzania
Imetolewa leo tarehe 15.11.2013 nami
Prof. Juma A.Kapuya
Mbunge – urambo magharibi
S.L.P 45 Kaliua Tabora
Simu 0784993930
Prof. Juma A.Kapuya
Mbunge – urambo magharibi
S.L.P 45 Kaliua Tabora
Simu 0784993930
No comments:
Post a Comment